Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Mabingwa mara 24 wa Ligi Kuu ya Tanzania bara timu ya Young Africans leo wanashuka katika dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam kucheza na timu ya Mgambo JKT kutoka mkoani Tanga katika muendelezo wa michezo ya VPL mzunguko wa nane.

Kocha mkuu wa Young Africans Marcio Maximo amesema anakiamini kikosi chake kitafanya vizuri katika mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya Mgambo JKT na kurudi katika nafasi mbili za juu za msimamo wa Ligi Kuu ya Vodacom.

Maximo amesema tumecheza vizuri mechi tatu zilizopita, matokeo ya mechi dhidi ya Kagera Sugar hatukugemea kupoteza mchezo, lakini naamini katika Uwanja wa Taifa tuna nafasi nzuri ya kupata ushindi na kucheza kandanda safi.

Aidha Maximo amesema wachezaji wote wanatambua umuhimu wa mchezo dhidi ya Mgambo JKT kesho, nawaheshimu wapinzanii wetu ni wazuri kwa sababu hii ni Ligi na kila mmoja anahitaji pointi tatu muhimu tumejiandaa kupata ushindi.

"Nina kikosi kizuri chenye ushindani, kwanza tumeshinda Ngao ya Jamii, pili tunategemea kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom na kuingia hatua ya makundi kwenye michuano ya kombe la washindi barani Afrika mwakani" amesema Maximo.

Kuelekea mchezo wa kesho dhidi ya Mgambo JKT, Kikosi cha Young Africans kimeingia kambini jana jioni katika hoteli ya Valley View kujiandaa na mchezo huo ambapo wa wachezaji wawili Nahodha wa timu Nadir Haroub "Cannavaro" na mshambuliaji Hussein Javu wataukosa mchezo huo.
 
Kocha Marcio Maximo amewaomba wapenzi, wanachama na washabiki wa Young Africans kujitokeza kesho kwa wingi Uwanja wa Taifa kuja kuwapa hamasa vijana na kuwashangilia katika mchezo huo.
 RATIBA
Jumamosi Novemba 8
Stand United v Mbeya City         
Yanga v Mgambo JKT                
Mtibwa Sugar v Kagera Sugar               
Azam FC v Coastal Union           
Polisi Moro v Prisons
JUMAPILI Novemba 9
Simba v Ruvu Shootings             
JKT Ruvu v Ndanda FC

Standings


Rnk
TeamMPWDLGFGA+/-Pts

1
Mtibwa Sugar642092714

2
Coastal Union632185311

3
Azam631263310

4
Young Africans631275210

5
Kagera Sugar62315329

6
Mgambo JKT630345-19

7
JKT Ruvu621357-27

8
Ruvu Shooting621346-27

9
Simba SC60606606

9
Tanzania Prisons61326606

11
Ndanda6204810-26

12
Polisi Morogoro613257-26

13
Stand United613249-56

14
Mbeya City612325-35


Chapisha Maoni