Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


kuhusiana na kombe la dunia  2018 pia 2022,Madai zaidi yameibuka kuhusu ufisadi uliofanyika wakati wa shughuli ya kuwatafuta waandalizi wa kombe la dunia la mwaka miaka hiyo..

Nafasi hizo zilichukuliwa na Urusi pamoja na Qatar. Gazeti la Sunday Times nchini Uingereza limesema kuwa rais wa Urusi Vladimir Putin alihusika pakubwa wakati nchi yake ilipokuwa ikitafuta nafasi hiyo na hata alimuomba rais wa FIFA Sepp Blattter kuisaidia kupata kura.

Pia kuna madai kuwa nchi ya Qatar ilitumia ushawishi wake katika sekta ya gesi kupata kura kupitia kandarasi za kibiashara.

Urusi na Qatar zimekana kuhusika kwenye vitendo hivyo na ziliondolewa lawama na shirikisho la soka duniani FIFA hivi majuzi.


Chapisha Maoni