Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Na Alex Mapunda,Iringa
WACHEZAJI wa timu ya soka ya Lipuli wamepewa likizo ya siku 10,kabla ya kurudi kambini ili kujiandaa na mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza.

Katika mzungunguko wa kwanza Lipuli ilimaliza katika nafsi ya tatu  Nyuma ya Maji Maji na Friends Rangers toka Jijini Dar ambapo bado wanakibarua kigumu cha kupambana zaidi kwa kuwa msimu huu kuna makundi mawili na kila kundi zitapanda daraja timu mbili.
Akizungumza na Jelamba viwanjani katibu msaidizi wa Lipuli Ronjino Malambo alisema  wameamua kutoa likizo kwa wachezaji ili kwenda kusalimia familia zao huko uongozi wa timu ukijipanga kuziba mapengo yaliyojitokeza mzunguko wa kwanza.

“sasa ni wakati wa kuangalia mapungufu yaliyojitokeza katika timu yetu hasa katika sehemu ya kiungo na ushambuliaji na tunatarajia mzunguko wa pili tutafanya vizuri zaidi ya hapo,kikubwa ni kupanda ligi kuu”alisema malambo.
Wadau na mashabiki  wa kandanda mkoani hapa wanakiu ya kuona ligi kuu ikichezwa katika uwajana wa nyumbani na tegemeo pekee ni kwa Lipuli au Kurugenzi.


Chapisha Maoni