Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Mmoja wa viongozi wa kamati ya utendaji ya klabu ya Yanga amesema, Maximo ataondoka nchini ndani ya siku tatu baada ya kukubaliana na uongozi.
"Si kwamba amefukuzwa, lakini ni makubaliano kwamba anaondoka.
"Ni kweli, lakini msitake kulikuza hili jambo ionekane kama tumemfukuza," aliuliza na alipotakiwa kujua mrithi ni nani, alikataa kusema.
Lakini taarifa nyingine zimeeleza Yanga inamrejesha Kocha Hans van der Pluijm.
"Suala la kocha gani tunaomba msubiri, hilo la Pluijm aliyekuambia nani, naomba mtuache kwanza," alikuwa mkali kiongozi huyo.
 USAJILI DILISHA LIMEFUNGWA.
Mwadui imesajili wachezaji wanne katika siku moja ya mwisho ambao ni Razak Khalfan kutoka Coastal Union, Uhuru Selemani, Joram Mgeveke (Simba) na Mohammed Mkweche.
Lakini wakongwe Simba na Yanga nao wamefunga dirisha kwa kulamba bingo.

Yanga imemnasa Amissi Tambwe aliyekuwa ameachwa Simba na kumsainisha mwaka mmoja, huku Simba ikimalizana na beki mbishi, Mohammed Kessy ambaye amesaini mwaka mmoja na nusu hukuStand United imenufaika na usajili wa Haruna Chanongo. 
ENDELEA KUSOMA JELAMBA VIWANJANI KWA TAARIFA ZAIDI 


Chapisha Maoni