Na Alex Mapunda,Iringa
TIMU ya soka ya Lipuli ya Iringa Inatarajia kuingia
kambini rasmi maeneo ya veta Iringa Mjini ili kujiwinda na
mzunguko wa pili wa ligi daraja la kwanza inayotaraijia kukata utepe hivi karibuni.
Baadhi ya wachezaji wanaotokea dar tayari walikuwa
kambini jijini Dar es salam eneo la karume na wanataraji kuwasili mkoani Iringa
ili kuungana na wezao toka maeneo tofauti pamoja na wachezaji wapya waliosalijiliwa
msimu huu kwaajili ya kambi ya pamoja.
“tumesajili wachezaji wapya watano ambao wataziba
mapengo yaliyojitokeza msimu uliopita kama Ripoti ya mwalimu ilivyokuwa
ikijieleza,leo jumatano wachezaji wote wanaanza kambi rasmi na maandalizi yote
yanaenda vizuri sana”,Alisema Ronjino Malambo.
Vile vile ronjino malambo aliwapongeza wadau na
mashiki mkoani hapa kwa sapoti kubwa mbayo wanaitoa kwa timu ya Lipuli ambapo
amewaomba waendelee kuiunga mkono zaidi timu hiyo kwa manufaa ya wanairinga
wote.
Lipuli inanafsi kubwa ya kupanda daraja msimu huu
kama wanadau,mashabiki pamoja viongozi watakuwa kitu kimoja katika kuijenga
Ripuli.
Chapisha Maoni