Mechi ya Nani Mtani Jembe namba 2
itafanyika kesho siku ya jumamosi katika dimba la Uwanja ambapo itawakutanisha
Young Africans Sports Club dhidi ya Simba SC huku timu zote zikitarajiwa
kuwatumia wachezai wao wapya zilizowasajili katika kipindi cha dirisha dogo.
Kikosi cha mbrazil Marcio Maximo tayari
kimeshawasajili wachezaji wawili kiungo Emerson de Oliveira kutoka nchini
Brazil na mshambuliaji mkongwe na mzoefu wa hali ya juu Danny Mrwanda ambao
wanatajiwa kuongeza nguvu katika mchezo huo wa kesho.
Young Africans chini ya kocha mkuu
Marcio Maximo inaendelea na mazoezi katika Uwanja wa Boko Veterani huku
wachezaji wote 26 waliongia kambini wakiendelea kujifua kuwa fit kwa ajili ya
mchezo huo wa siku ya jumamosi.
Huu ni mchezo wa pili wa Nani Mtani
Jembe kuzikutanisha timu hizi kwani katika mchezo wa awali uliofanyika mwaka
jana, Young Africans ilipoteza kwa mabao 3- 1, na kocha Maximo pamoja na
wachezaji wake wamejiandaa kuhakikisha safari hii wanapata ushindi kwenye
mchezo huo.
Kocha Maximo amesema vijana wake
wote wapo kwenye hali nzuri kuelekea mchezo huo, ambapo mchezaji pekee majeruhi
ni Jerson Tegete ambaye alipata majeraha hayo katika mchezo wa kirafiki dhidi
ya timu ya Vipers kutoka nchini Uganda.
Kwa
upande mwingine Habari
nzuri kwa mashabiki wa Simba, kiungo mkabaji wa timu hiyo, Jonas Mkude, ameanza
mazoezi baada ya kupona malaria iliyomuweka nje ya uwanja kwa wiki moja kwa
ajili ya matibabu.
Kiungo huyo alishindwa
kumalizia mazoezi ya wiki iliyopita kwenye Uwanja wa TCC, Chang’ombe jijini Dar
es Salaam baada ya kutapika kabla ya kufanyiwa vipimo na kukutwa na malaria na
kuanza dozi.
Katika mazoezi ya jana
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Chuo cha Ualimu hapa Unguja, Zanzibar kiungo
huyo alionekana akianza mazoezi mepesi ya binafsi kukimbia akiwa chini ya
uangalizi wa daktari, Yassin Gembe.
Gembe alisema Mkude amepona
kabisa na mechi ya kesho Jumamosi ya Nani Mtani Jembe dhidi ya Yanga atakuwepo
uwanjani kama kocha ataamua kumtumia.
“Mkude kama unavyomuona hii
leo (jana) asubuhi ameanza mazoezi mepesi ya binafsi kwa ajili ya kurudisha
afya yake ya kawaida, ameanza mazoezi mepesi na baadaye akafanya ya nguvu
pamoja na wenzake.
“Ametokea kwenye malaria,
hivyo ni lazima aanzie na mazoezi mepesi ili hali ya kawaida irejee, kocha
akiamua kumtumia ni ruksa. Tofauti na Mkude hakuna majeruhi mwingine,” alisema
Gembe.
Chapisha Maoni