NA Alex Mapunda,Iringa
BONDIA toka songea maarufu kwa jina la dume la Simba anatarajia
kupanda ulingoni kupambana na Benki mwakalebera katika pambano la raundi 8
litakalopigwa njombe Tarehe 7 siku ya jumapili.
Katika pambano hilo ambalo linatarajia kuwa
na upinzani mkubwa pia kutakuwepo na mpambano ya utangulizi ambapo Bondia Alex
kiwawa atamenyana na Daudi Joseph Toka Morogoro,Ally Bobu wa njombe atapambana
na Furaha Mapepe kisha Poul mavisu wa Songea atavaana na Damas toka njombe.
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI mwalimu
Simba la Dume toka Songea Musa Omari alisema wapo kwenye maandalizi mazito ili
kuhakikisha Simba dume anaibuka kidedea katika mpambano huo.
“tunapigana ili kuhakikisha songea wanapatikana wapiganaji wengi wa ngumi kwa
kuwa mchezo wa ngumi ni mchezo ambao unashika kasi duniani kwa sasa hivyo itasadia vijana wengi
kupata ajira.
Pia musa omari alisema siku ya sikuu ya noeli
mwenzi huu anatarajia kupanda ulingoni kuvaana na Kosmas cheka pambano ambalo
litapigwa songea mjini.
Chapisha Maoni