Mshambuliaji matata wa kilabu ya Gor
Mahia nchini Kenya Dan Sserenkuma aihama kilabu hiyo na kujiunga na Simba SC ya
Tanzania
Aliyekuwa Mshambuliiaji wa mabingwa
wa soka nchini Kenya Gor Mahia Dan Serenkuma amejiunga na kilabu ya Tanzania
Simba SC.
Raia huyo wa Uganda alijiunga na
kilabu hiyo ya Ligi ya Vodacom na kutamatisha kazi yake ya miaka mitatu katika
ligi ya Kenya ambapo alianza kwa kuichezea Nairobi City Stars kabla ya kujiunga
na Gor ambapo alikuwa kiungo muhimu katika ushindi wa ligi mara mbili.
''Nimefurahia miaka miwili na nusu
katika kilabu ya Gor Mahia,lakini huu ndio wakati muhimu wa kuaga.Tumefurahia
nyakati maalum na mafanikio pamoja,na habiki wamenisaidia sana hususan wakati
mgumu'',Mfungaji huyo wa mabao mengi katika ligi ya Kenya aliandika katika
mtandao wake wa Twitter.
''Ningependa kumshukuru kila mtu
katika usimamizi wa kilabu kwa kunipa fursa muhimu ili kuonyesha kipaji changu.
Dan Sserenkuma
Mchezaji huyo wa kimataifa katika
timu ya Uganda Cranes alipigwa picha katika mtandao wa kilabu hiyo akifanyiwa
majaribio pamoja na kupimwa afya na sasa anatarajiwa kujiunga na wachezaji
wenzake katika barabara ya Msimbazi mjini Daresalaam tayari kwa maandalizi ya
mechi za ligi ya Tanzania.
Wakati huohuo imebainika kwamba
Kilabu ya Gor Mahia ilishindwa kumzuia mchezaji huyo.
Duru zimearifu kuwa mchezaji huyo
aliandamwa na kilabu ya Gor mahia kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba
alitarajiwa kujiunga na Simba.
Lakini Gor Mahia haikuwasilisha ombi
lolote la fedha kwa kuwa mchezaji huyo tayari alikuwa ameweka kandarasi yenye
thamani ya shilingi millioni 3 pamoja na mshahara wa ksh.250,000 kwa mwezi na
kilabu hiyo ya Tanzania ambapo atajiunga na mchezaji mwengine wa Gor Mahia
Mungai Kiongera.
Chapisha Maoni