Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Na Alex Mapunda,Iringa
SAFARI ya chuo kuku cha iringa ya kwenda kushiriki michuano ya vyuo vikuu Kampala Uganda ambayo inatarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 16 mwenzi huu imeota mbawa sababu kubwa ekielezwa ni fedha.

Wakizungumza na JELAMBA katika nyakati tofauti baadhi ya wachezaji  ambao walikataa kutaja majina yao walisema kuwa kutokwenda kushiriki mashindano makubwa kama hayo kwa chuo kikuu cha Iringa ni haibu kwa  kwa chuo kwa kuwa michuano hii inatoa fursa kwa wanachuo mbali mbali kufahamiana na kutengeneza channeli za hajira.

“tunajifunza mengi kupitia michezo hii,kuto kushiriki michuano hii tumekosa haki ya msingi ambazo wezetu wamepewa chuo kifikiria vizuri kuhusu sisi kwenda Uganda na umuhimu wa michano yenyewe kwa sisi na chuo”
“hatujatendewa haki kabisa bora wangesema mapema kuriko kutuacha tufanye mazoezi hadi dakika ya mwisho,sisi tumeacha kusoma kwajili ya kufanya mzoezi ya kwenda Uganda,wametuumiza sana”walisema wanafunzi hao.

Hata hivyo,Mwaka uliopita chuo kikuu cha Iringa kiliambulia patupu kwa michezo yote baada ya kutoka kapa bila medali hata moja,na safari hii wanaenda kujalibu bahati yao ili kuona kama wanaweza kuambulia japokuwa medali ya shaba.


Chapisha Maoni