Soka la Tanzania kwa miaka ya hivi karibuni
limeonekana kukosa mwelekeo baada ya
timu ya taifa kufanya vibaya pamoja na vilabu katika mashindano mali mbali
suala ambalo wadau na wachambuzi wengi wa soka ndani na nje ya Tanzania
wamekuwa wakilizungumzia sana.
Mara nyingi viongozi wa vilabu bila kusahau Tff
wanaraumiwa sana na mashabiki pamoja na wadau wa soka hapa nchini kwa kuendesha
mpira kisiasa badala ya kuendesha
kisayansi kama ilivyo kwa nchi za wenzetu hali ambayo imepelekea vilabu vyetu na timu
ya taifa kufanya vibaya hasa kwa kipindi cha mika 15 ya hivi karibuni.
Lakini ukweli ni kwamba sio viongozi peke yao ndio
wametufikisha hapa bali ni kukosekana kwa uzalendo toka kwa Viongozi,wanachama pamoja na wachezaji
ambao wameshindwa kuweka maslai ya taifa
mbele na Badala yake wametanguliza maslai yao na kulifanya soka la Tanzania
kuendelea kubaki kuwa ni kichwa cha mwendawazimu,Tusilaumiane au kunyosheana
vidole wakati tunajenga nyumba moja.
Kazi ya viongozi ni kuongoza,kazi ya wachezaji ni
kucheza mpira na kazi ya wanachama ni kuchangia timu kwa hali na mali lakini
inanvyoonekana kuwa viongozi wanaingilia
kazi ya wachezaji au wachezaji kuingilia kazi ya wanchana tayari linakuwa ni
Tatizo na mwisho wa siku lazima itokee migogoro ambayo itapelekea timu kuyumba.
Kwa mara ya mwisho Tanzania kushiriki michuano ya
mataifa huru ya Afrika ilikuwa ni mwaka 1980 inchini Nigeria ni takribani miaka
34 imepita sawa na umri wa mtu mzima,hii ni aibu kubwa kwa taifa kama la Tanzania
ambalo watu wake wanapenda sana michezo.
Ili kuendeleza mpira wa Tanzania watu wote bila kujali wazee au vijana lazima
watambue kuwa maendeleo ya mpira wa nchi ya hii yapo mikononi mwao na sio
mikononi mwa wachache,kama nchi itajitambua tunaamini viwanja vitajengwa,shule
za michezo zitajengwa pia watu wenye taaluma ya mpira ndio watakabidhiwa nyazifa zote zinazohusu mpira
wa
miguu,tofauti na ilivyo hivi sasa.
Chapisha Maoni