Kocha wa Arsenal Arsene Wenger amesema anakiogopa kichapo cha mabao 5-1 dhidi ya timu yake kilichotokea wakati wa mechi kati ya
Liverpool na Arsenal msimu uliopita
Kocha wa kilabu ya Arsenal Arsene
Wenger amekiri kwamba anaogopa kichapo cha 5-1 alichokipata wakati timu yake
ilipochuana na Liverpool msimu uliopita, lakini akaongeza kuwa hatarajii
kichapo kama hicho wakati timu hizo mbili zitakapokutana siku ya jumapili.
Arsenal ilikuwa imefungwa mabao 4-0
kufikia dakika ya 20 wakati wa mechi hiyo iliochezwa Anfield huku Liverpool
ikiongozwa na mshambuliaji hatari ambaye ameihama kilabu hiyo Luis Suarez.Mechi
hiyo ilikamilika ikiwa 5-1 dhidi ya Arsenal.
Lakini meneja huyo wa Arsenal
anaamini mengi yamebadilika katika kipindi cha miezi 10,ikiwemo kuondoka kwa
Suarez na jeraha la mshambuliaji Daniel Sturridge na mafanikio yake ya
kumsajili Alexis Sanchez kutoka Barcelona mbele ya Breanda Rodgers.
Walikuwa wazuri sana katika safu ya
mashambulizi,lakini msimu huu wamefunga mabao 19 pekee,hawana tena moto wa
kufunga mabao waliokuwa nao.
Walianza kwa mori siku hiyo na sisi
tulishindwa kujibu mashambulizi yao.
Kila mechi unayoshindwa inakua kovu
katika moyo milele.Lakini tuna kumbukumbu nzuri katika uwanja wa liverpool.
Tulishinda mechi nyingi sana katika
uwanja huo,lakini utakumbuka kwamba juma moja baadaye tuliweza kuishinda timu
hiyo hiyo tulipocheza nayo nyumbani katika kombe la FA.'
http://www.bbc.co.uk
Chapisha Maoni