Lionel Messi ameambiwa kwamba kuna
mkataba wa miaka sita kutoka kwa kilabu ya Chelsea unaomngojea.
Duru za karibu na mchezaji huyo wa
Barcelona zinaarifu kuwa Chelsea imeweka wazi kwamba iko tayari kutoa kitita
cha pauni millioni 200 kumnunua nyota huyo.
Vilevile The Blues imedaiwa kwamba
iko tayari kulipa mahitaji yake ya mshahara ambayo huenda yakaongeza kiwango
hicho mara mbili.
Mnamo mwezi Novemba kocha wa Chelsea
Jose Mourinho alikana habari zinazoihusisha kilabu hiyo na Messi,lakini katika
kilabu ya Barcelona kumekuwa na mgogoro tangu wakati huo na ripoti kutoka
Uhispania zinasema kuwa mchezaji huyo amekuwa akizozana na muajiri wake Luis
Enrique.
Inadiwa kuwa Mesi hakushiriki katika
mazoezi ya siku ya jumatatu huku Enrique akishindwa kukana mgogoro uliopo kati
yake na Messi.
Chapisha Maoni