Na Alex Mapunda,Iringa
Baada ya Polisi kusimamisha mkutano mkuu wa Lipuli Jumapili iliyopita kwa madai
kuwa viongozi wa timu hiyo hawakufuata taratibu, mkutano huo sasa umepangwa
kufanyika kesho kutwa wikendi hii katika
ukumbe wa veta mkoani hapa.
Akizungumza na JELAMBA VIWANJANI
katibu Msaidizi wa Lipuli Ronjino Malambo alisema kuwa Polisi waliwashauri
kuhairisha mkutano huo kwa kuwa hawakufuata taratibu za kiusalama ili kuepuka
madhara endapo zingetokea vurugu zozote katika mkutano huo.
“wote viongozi na wanachama ambao
tulifika kwa moyo mmoja na sasa
tunafuata taratibu na mkutano huo utafanyika saa nne Asubuhi siku ya jumapili
kama ambavyo tulipanga hapo awali”alisema Malambo.
Akielezea
mkutano huo mwenyekiti wa Lipuli AbuuMajeki alisema lengo kubwa na mkutano huo
ni kuzungumzia matatizo ya Lipuli kushindwa kupanda daraja pia kumtatufa
aliyesababisha timu hiyo isipande ligi kuu.
“Kutokana
na wanachama kudai mara kwa mara mkutano mkuu wa Lipuli ili kujadili nani
mchawi wa timu mimi nimeamua mkutano ufanyike siku ya Jumapili japo kuwa tarehe
rasmi ya mkutano bado haijafika”
“Namegiza
katibu wangu kuitisha kamati ya utendaji ili kujadili kuhusu mkutano huo lakini
suala la kufanya mkutano jumapili mimi nimeshatanga mkutano lazima ufanyike
siku ya Jumapili,alisema Majeki.
Majeki
aliongeza kuwa wanachama wote wenye kadi na wasiokuwa na kadi wajitokeze kwa
wingi katika uwanja wa Samora ili kusikiliza kitakachotokea siku hiyo ambapo kama
itabainika Abuu Changawa ni chanzo cha Lipuli kufanya vibaya atatangaza
kujiuzulu na kama sio yeye basi hatua kali zitachukuliwa kwa wale wote
watakaobainika kuiujumu Lipuli.
Chapisha Maoni