Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





 

MKAZI wa Kakiika wilayani Mbarara nchini Uganda, Deus Ruhinda amejinyonga baada mkeka wake kuchanika kufuatia Arsenal kufungwa bao 3-1 dhidi ya monaco hivi karibuni.




Ruhinda ambaye alikuwa akifanya kazi manispaa ya kasese ameamua kukatisha maisha yake baada ya  kukosa sh 500,000 ambazo angezipata kutokana na kubeti kama Arsenal angeshinda dhidi ya Monaco. 
 
Taarifa kutoka kwa majirani zinasema kuwa Ruhinda alikutwa tarehe 28 akiwa amejinyonga katika shamba la ndizi kwa kutumia mti wa Avocado ambao ulikuwepo katika shamba hilo.

Mashaidi wa tukio hilo walisema kuwa pesa ambazo alibetia zilitokana na Boda boda pia, zingine zilikuwa za bosi wake huko kisese hivyo alipatwa na presha baada ya mkeka kuchanika na kukosa mtu wa kumlipia deni lake.


Chapisha Maoni