Mchezo wa kirafiki wa Kimataifa
uliofanyika jana jumapili jijini Mwanza kwenye Uwanja wa CCM Kirumba kati ya
wenyeji timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) dhidi ya timu ya Taifa ya
Malawi (The Flames) umengiza jumla ya tsh 72.839,000 kutokana na idadi ya
washabiki 15,762 waliokata tiketi kushuhudia mchezo huo.
Mgawanyo wa mapato kwa mchezo hu ni VAT
18% sh. 11,111,103, gharama za tiketi sh. 3,203,700, gharama za mchezo (15%)sh.
8,778,639, Uwanja (15%) 8,778,639, CAF (10%) sh. 5,852,426 na Shirikisho la
Mpira wa Miguu nchini TFF (35%) sh. 35,114,560.
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini
inatoa shukrani kwa chama cha soka mkoa wa Mwanza (MZFA) kwa ushirikiano
wao katika kufanikisha maandalizi ya mchezo huo, waandishi na vyombo vya habari
mbalimbali kwa sapoti waliyoitoa kwa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars)
Katika mchezo huo Taifa Star ilitoka
sare ya bao 1- 1 dhidi ya The Flames, bao la wageni lilifungwa na Mecium Mhone
kabla ya na Mbwana Samatta kuisawazishia Tanzania.
Chapisha Maoni