Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Afisa mkuu mtendaji wa Arsenal, Ivan Gazidis ametangaza wana Gunners lengo lao muhimu zaidi si kunyakua kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Mzaliwa huyo wa Afrika Kusini alikuwa anahotubia kongamano lililoandaliwa na shirika la ufadhili, Kick It Out ambalo linapigania kuondolewa kwa ubaguzi wa rangi katika kandanda ya Uingereza.
“Tukizungumzia mwisho wa safari, kushinda Ligi ya Mabingwa sio lengo kuu kuliko kuwaridhisha mashabiki wetu. Azima yetu ni kuwapatia wafuasi wetu sababu ya kupata shime na klabu chao kama jukumu letu,” Gazidis aliendelea.
Kinara huyo wa zamani wa ligi kuu ya soka Marekani, MLS, alijiunga na Gunners 2006 huku timu hiyo ikicheza fainali ya kipute hicho cha kifahari mara ya mwisho 2006 kabla ya kuondolewa katika awamu ya 16-bora kila mwaka uliofuata.
“Tunapokea shutuma kali lakini tuna wahudumu hapa ambao wanahusika vilivyo na kufanisisha malengo yetu ya miaka mingi ijayo na hatubanduki kutoka mwelekeo huo kwa hisia za kila kinachotukia kila siku,” aliongeza.
Arsenal wanashikilia nafasi ya tatu kwenye msururu wa ligi Premier ya Uingereza nyuma ya Chelsea na Manchester City huku wakionekana kufuzu Ligi ya Mabingwa huku wakiwania na


Chapisha Maoni