Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kocha wa Barcelona, Luis Enrique amesisitiza hakuna timu yoyote duniani inaweza kumudu makali ya washambuliaji wake nyota, Lionel Messi, Luis Suarez na Neymar mbele ya lango baada ya kikosi chake kuadhibu vikali Getafe 6-0 katika ngoma ya La Liga.
Watatu hao wamezamisha magoli 102 kwa ujumla katika mashindano yote musimu huu baada ya Messi na Suarez kupata mawili kila mmoja na Neymar kuchangia lingine huku kiungo maarufu Xavi akitikisa nyavu kufungua mwanya wa alama tano kileleni mwa ligi kuu Uhispania Jumatano usiku.
“Ni siku nyingine ya kushukuru timu hii kwasababu mechi kama hizi zinaweza kuwa ngumu kwa urahisi na tulihitaji mwanzo moto kama wa leo.
“Kulikuwa na baadhi ya sababu za kusema hakuna anayeweza kukomesha timu hii kwani tulipata nafasi nyingi na kupachika mabao ya hali ya juu. Sikumbuki mechi ya Barca au timu ingine yeyote ina makali kama haya mbele ya lango,” Enrique alisema.
Washindani wao wa karibu, Real Madrid wana nafasi ya kufunga tofauti hadi pointi mbili Jumatano usiki watakapomenyana na wanyonge Almeria lakini miamba hao wa Ulaya hawana kipawa cha kuzuia Barcelona kutawazwa mabingwa wa La Liga iwapo watatamba katika mechi zote nne zinazosalia.
Cordoba, Real Sociedad, mabingwa watetezi Atletico Madrid na Deportivo la Coruna ndio wanaosalia kukumpana na tisho la majitu hao wa Catalunya huku Madrid wakisalia na vivumbi vigumu dhidi ya Sevilla na Valencia ambao wanawania kufuzu Ligi ya Mabingwa Ulaya musimu ujao.
“Hatutakazua juhudi kwani tunaelewa tunajitegemea sisi wenyewe dhidi ya washindani wakuu kama Real Madrid ambao watapigania taji hili hadi mwisho. Tuna changamoto ya kuendeleza mkimbio wetu sasa na kumakinika vilivyo,” Enrique aliongeza.


Chapisha Maoni