Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Habari za majuzi zaidi kuhusu kuhamia Italia kwa nyota huyo wa Ghana zilifichuliwa na gazeti la L'Equipe wikendi. Gazeti hilo lilisema mwana huyo wa kiume wa Abedi Pele ameamua kujiunga na Roma, lakini kwa sharti kwamba wafuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Kiungo huyo wa kati mshambulizi mwenye miaka 25 ni mmoja wa nyota kutoka Afrika ambao kwa sasa wamo sokoni.
Anasakwa na klabu kubwa kama vile Liverpool na Swansea City Uingereza, Borussia Dortmund, Wolfsburg, Bayer Leverkusen na Schalke Ujerumani, pamoja na Inter Milan na Roma nchini Italia.
Lakini naibu nahodha huyo wa Black Stars, ambaye mkataba wake wa sasa Olympique Marseille unamalizika mwisho wa msimu, anajulikana sana kuipa kipaumbele Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Inter tayari wako nje ya kupigania nafasi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya, huku Roma ambao wamekuwa hawachezi vyema kwa sasa wamo namabri tatu na ambayo ndiyo nafasi ya mwisho ya kufuzu kwa Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya katika Serie A, lakini wanakbiliwa na ushindani kutoka kwa Napoli walio alama tano nyuma, wakiwa na mechi moja hawajacheza, na zikiwa zimesalia mechi saba za kucheza ligini.


Chapisha Maoni