Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Chelsea watapiga hatua kubwa katika kukaribia kutwaa taji la Ligi Kuu ya Uingereza wakishinda ugenini dhidi ya Leicester City wanaokabiliwa na hatari ya kushushwa daraja Jumatano lakini Jose Mourinho anatarajia wapinzani hao wanusurike licha ya matokeo ya mechi hiyo.
Leicester, waliokuwa eneo la kushushwa daraja kutoka mwisho wa Novemba hadi wiki jana, waliondoka eneo hilo baada ya kushinda mechi zao nne zilizopita na Muoirnho alisema Jumatatu kwamba alijashangaa kwamba walijipata huko.
“Nilishangazwa na hali yao mbaya. Kwangu hiyo ni timu nzuri na yenye wachezaji wazuri. Tulicheza dhidi yao mapema kwenye msimu Stamford Bridge, na mara moja nilihisi ubora wa timu hiyo.
“Sijashangaa kwamba wameondoka eneo la kushushwa daraja. Na sitashangaa wakisalia ligi kuu. Ninafikiri watanusurika.”
Malengo ya sasa ya Chelsea ni tofauti kabisa nay a Leicester , huku mabingwa watarajiwa wa Mourinho wakihitaji alama sita pekee kushinda taji. Upande mwingine Leicester wanahitaji alama nyingi kadiri wawezavyo kukwepa kurejeshwa ligi ya Championship.
Sehemu ya chini ya ligi, klabu saba zimetenganishwa na alama tisa lakini Leicester ndio wanaoonekana thabiti kwa sasa na wamo alama moja juu ya maeneo ya kushushwa ngazi ambayo yanakaliwa na Sunderland, Queens Park Rangers na Burnley, wakiwa na mechi moja hawajacheza wakilinganishwa na QPR na Burnley.
Mourinho anafikiri kuna mchezaji mmoja "wa maana sana kwangu” atakayesaidia Leicester kunusurika.
Kiungo wa kati wa Argentina Esteban Cambiasso alikuwa Inter Milan klabu hiyo ilipokuwa ikinolewa na Mourinho iliposhinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya 2010, na kocha huyo Mreno alimsifu mchezaji huyo wake wa zamani Jumatatu.
"Cambiasso alikuwa kwenye timu yangu stadi Inter kwa hivyo yeye ni mmoja wa wachezaji ninaodhamini sana. Amefaa sana Leicester msimu huu na nina furaha.
“Sikushangaa kwamba alikuja hapa Uingereza. Ninajua kwamba yeye ni mtu wa Inter daima, lakini pia ni mtu wazi anayependa kujaribu kwingine.
“Ikizingatiwa kwamba ni mchezaji mwerevu sana na huzungumza Kiingereza kwa ufasaha, haikunishangaza alipokuja hapa Uingereza.
"Bila shaka, msimu ujao atachezea Leicester katika Ligi Kuu ya Uingereza."


Chapisha Maoni