Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.



Kocha Mkuu wa Simba, Goran Kopunovic amesema amemuacha beki Hassan Kessy kwa kuwa hayuko fiti.

Kopunovic amesema Kessy hakufanya mazoezi na wenzake kwa zaidi ya wiki moja.
Hivyo isingekuwa lahisi kumjumuisha katika kikosi kinachokwenda kuivaa Mbeya City kwenye Uwanja wa Sokoine.
“Amekuja siku moja kabla hatujaondoka, alifanya mazoezi kidogo tu. Kocha hawezi kuamini kwa hisia kwamba niamini Kessy ana mazoezi.
“Kocha makini ataamini baada ya kuona, unawatumia watu unaowaona wanafanya pamoja nawe hayo mazoezi.
“Lakini hakuna kitu kingine, zaidi ni masuala ya kiufundi na tunataka kushinda mechi hiyo licha ya ubora wa Mbeya City,” alisema Kopunovic.

Kessy hakuwa kambini baada ya kuanzisha mgomo baridi akishinikiza uongozi ummalizie kitita chake cha Sh milioni 5 pamoja na fedha ya pango.


Chapisha Maoni