Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.




mashabiki-yanga


YANGA SC imetaja viingilio vya mechi yao ya hatua ya 16 ya kombe la Shirikisho itayopigwa keshokutwa uwanja wa Taifa Dar es salaam dhidi ya Etoile du Sahel ya Tunisia.

Mkuu wa Idara ya habari na mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro,  leo amekutana na waandishi wa habari makao makuu ya klabu hiyo, Mitaa ya Jangwani, Kariakoo Dar es salaam na kusema kuwa kiingilio cha chini katika kipute hicho ni shilingi elfu tano (5,000) kwa vitu vya rangi ya bluu na kijani.
 Etoile-du-Sahel
Viti vya rangi ya Chungwa, Muro amesema kiingilio ni shilingi elfu kumi (10,000) wakati VIP C ni shilingi elfu ishirini (20,000).

Aidha Muro ameongeza kuwa VIP B ni shilingi elfu 30,000 na VIP A ni shilingi elfu arobaini (40,000).
Tiketi zitauzwa uwanja wa Karume, Billicanas, Feri, Buguruni Sheli, Dar Live, Stand ya mabasi ya Ubungo, Uwanja wa Taifa, makao makuu ya Yanga makutano ya Twiga na Jangwani, Mwembe Yanga na Tandika.
Yanga wameweka kambi Hoteli ya Tansoma Dar es salaam na wanaendelea na mazoezi uwanja wa Karume na jioni hii wapo uwanja wa Taifa.
Etoile du Sahel wanatarajia kuwasili saa 9:00 alfajiri ya kesho na jioni watafanya mazoezi uwanja wa Taifa



Chapisha Maoni