Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 


 

 

 Mashabiki 7 wa Simba ya jijini Dar es Salaam, wamefariki dunia na wengine 18 wamejeruhiwa baada ya basi lao dogo aina ya Coaster walilokuwa wakisafiria kuelekea mkoni Shinyanga, kuacha njia na kupinduka eneo la Kwa Makunganya barabara kuu ya Morogoro - Dodoma. Mashabiki hao walikuwa wanaenda Shinyanga kuishangilia timu yao katika mchezo wa ligi kuu bara unaotarajia kuchezwa kesho April 4, 2015 kwenye Uwanja wa Kambarage kati yao na Kagera Sugar. Miongoni mwa watu hao waliofariki dunia walikuwa wanaume sita na mwanamke mmoja, huku watano wakifariki eneo la tukio na wawili wakifariki baada ya kufikishwa hospitali ya mkoa walikolazwa majeruhi.
 Askari polisi na baadhi ya mashabiki waliokuwamo katika gari hiyo, wakiwa eneo la tukio.

 Gari hilo baada ya ajali.


Chapisha Maoni