Kauli hiyo ya Pluijm imetolewa wakati Yanga ikiondoka leo alfajiri kwenda Zimbabwe, tayari kwa mchezo wake wa marudiano dhidi ya Platinum utakaofanyika kwenye Uwanja wa Mandava mjini Zvishavane kesho.
Timu hiyo kibindoni ina akiba ya ushindi wa mabao 5-1 ilioupata katika mchezo wa kwanza uliofanyika Dar es Salaam wiki mbili zilizopita.
Mdachi huyo aliitaka Yanga kuhakikisha inaweka rekodi kwenye mashindano ya kimataifa na kuzima maneno ya watu ambao wamekuwa wakiisema klabu hiyo kuwa haina lolote, inafanya vizuri kwenye ardhi ya Tanzania.
Baadhi ya wakosoaji wamekuwa wakidai Yanga inachukua ubingwa wa Bara mara kwa mara, lakini kwenye mashindano ya kimatifa hutolewa mapema.
Wakati huohuo, wajumbe wawili wa Yanga, Samuel Lukumay na Yusuphed Mhandeni waliotangulia Zimbabwe kukagua mazingira wamesema timu hiyo itafikia Bulawayo ili kukwepa hujuma katika mji wa Zvishavane na hoteli zake zinamilikiwa na viongozi wa Platinum.
Chapisha Maoni