Hatimaye baada ya mchakato wa muda mrefu, uliofanyika kwa umakini kwa kuzingatia vigezo vilivyowekwa hatimaye Shirikisho la Ngumi Tanzania (BFT) limepata wachezaji wa timu ya Taifa ya Ngumi 2015.
Katika mashindano ya kimataifa yaliyoshirikisha timu za taifa kutoka Uganda na Kenya, mashindano yaliyomalizika kwa mafanikio, Jumamosi ya tarehe 28.03.2015 uwanja wa Taifa wa ndani .
Mabondia waliochaguliwa kwa sasa taratibu za kuombewa ruhusa katika timu zao zinafanyika na taratibu hizo zitakapo kamilika watatakiwa kuanza mazoezi kabla ya tarehe 15.04.2015, kwa ajili ya kushiliki mashindano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa hasa mashindano ya Michezo ya Afrika (All African Games) Septemba 4-19. Brazzaville Congo. Na mashindano ya Ubingwa wa Dunia (AIBA World Boxing Championships) Octoba 5-18 Doha Qatar.
Mabondia waliochaguliwa kwa uzito wao ni kama ifuatavyo:-
49 kgs L/FLY
- Mohamed Mzeru –JKT
- Maulid Athumani-
- Ibrahim Abdalah – Magereza.
- Juma Ramadhani- Temeke
- Said Hofu- JKT
- Ahamad Furahisha- JKT
- Bon Mlingwa- JKT
- Elias Mkomwa- JKT
- Bosco Bakari- JKT
- Fabian Gaudence- NGOME
- Kassim Mbwitike- JKT
- Said Gulushad – JKT
- Seleman Bamtulah- JKT
- Ivan Mussa – Kagera
- Hamidu Halfan-JKT
- Alex Sitta- JKT
- Nuru Ibrahim- Magereza
Nakala kwenu kwa Taarifa.
Makore Mashaga
Katibu Mkuu (BFT)
Chapisha Maoni