Yanga imefanikiwa kuchanja mbuga katika michuano ya Kombe la
Shirikisho kwa jumla ya mabao 5-2 ikiwa ugenini nchini Zimbabwe.
Yanga
wamefuzu licha ya kufungwa kwa bao 1-0 dhidi ya FC Platnum katika mechi
iliyopigwa kwenye Uwanja wa Mandava ulio takribani Kilomita 200 kutoka
mji wa Bulawayo.
Mechi hiyo kali na ya kuvutia, wenyeji walipania kufunga mabao
manne ili wafuzu lakini ilishindikana.
Kocha Hans van der Pluijm alilazimika kumtoa mapema kinda Said
Juma ‘Makapu’ kutokana na kuonekana kuzidiwa na nafasi yake kumuingiza Kelvin
Yondani.
Kwa kuwa Yanga walifungwa katika kipindi cha kwanza, kipindi cha
pili, Mholanzi huyo aliamua kujaza viungo wengi zaidi.
Wingi wa viungo wengi, kulionyesha kuwanyima nguvu Wazimbabwe hao
hivyo kufanya Yanga icheze kwa kujiamini.
Pia kasi ya Platnum nayo ilipungua hivyo kuipa Yanga nafasi
kucheza vizuri.
Ngassa na Simo Msuva, pia walipoteza nafasi kadhaa ambazo zingeiwezesha kupata mabao. hata hivyo walikuwa tishio kwa mabeki hao wa Platnum.
Chapisha Maoni