Katika kuhadhimisha siku ya waandishi wa Habari chuo
kikuu cha Iringa ,leo ijumaa kuna Bonaza la michezo litakaloshirikisha michezo mbali mbali ambapo washiriki ni wanafunzi wote
wanaosomea uandishi wa Habari chuoni hapo.
Michezo hiyo
ambayo imeaza asubuhi hii ni Pamoja
na mchezo wa Kukuna Nazi,Mpira wa Miguu,wavu,Pete,Kikapu,Riadha, Kuvuta
Kamba Pamoja na Kuruka Kamba.
Vile Vile patakuwepo
na Mashindano ya Kucheza Mziki,kuimba ,kukimbia Ndani ya Magunia,Kukimbiza Kuku,Kukimbia na
yai kwenye kijiko pamoja na Kunywa Soda.
Akizungumza na Jelamba viwanjani Mwenyekiti wa
Mashindano hayo Shedrack Mgaya
amesema lengo kubwa la
Bonaza ni kujenga Umoja kwa wanafunzi wote pamoja na
kuhamasisha michezo.
“,waandishi wa Habari lazima tutambue kwamba ili kuendeleza michezo lazima tuwe katika mstari wa mbele kuhamasisha
michezo, ni kitu ambacho kipo ndani ya
uwezo wetu wakati mwingine,inatulazimu kuandaa mabonza mara kwa mara ili kutoa
elimu kwa jamii”Alisema Mgaya.
Katika Bonaza Hilo washindi watapata
Soda,Peni,Biskuti pamoja na Soksi kama
motisha kwa kushiriki
Chapisha Maoni