Polisi nchini Uswiss wamewakamata
maafisa sita wa vyeo vya juu wa shirikisho la soka duniani (FIFA) kwa
tuhuma za rushwa.Polisi hao wamewakamata maafisa hao leo asubuhi saa 12
kukiwa ndio kumekucha baada ya kuwavamia maafisa hao kwenye hoteli
waliokuwa wakiishi.
Maafisa hao waliokamtwa ni pamoja
na makamu wa Rais wa FIFA, Jeffrey Webb na FIFA wamethibitisha
hilo.Polisi wamewakamata maafisa hao kufuatia ombi la Shirika la
Upelelezi la Marekani (Federal Bureau of Investigation (FBI)) wakamatwe
kwa kufanya na kupokea rushwa miaka ya 1990 kwenye mabara ya Amerika ya
Kaskazini ikiwemo nchini Marekani ambapo mashindano ya soka yalifanyika
ambapo malipo ya pesa yalifanyika kwenye benki za Marekani na pia kwenye
bara la Amerika Kusini.
Mwanasheria Mkuu wa Marekani
kutoka wilaya ya New York Mashariki ambaye aliongoza uchunguzi wa sakata
hilo, aliiomba ofisi ya jaji Mkuu wa Uswizi aruhusu wakamatwe
maofisa hao.
maofisa hao.
Maofisa hao wanatuhumiwa pia
kutakatisha pesa haramu.Maofisa hao sasa bado wapo chini ya mikono ya
polisi wa Uswizi lakini wanaweza kusafirishwa kwenda Marekani kwa
mamlaka za nchi hiyo kwa FBI kujibu masuala hayo ya rushwa na wanaweza
kushtakiwa.
FIFA wamesema Rais wao Sepp
Blatter hajakamatwa.Hilo ni pigo kubwa kwa FIFA ambao ijumaa ya wiki hii
kesho kutwa watafanya uchaguzi wa Rais wa shirikisho hilo.Na imetikisa medani ya soka kwa ujumla.Maafisa
hao bado wanaendelea kuhojiwa na polisi huku wakiulizwa jinsi kura
zilivyopigwa kupata nchi zitakazoandaa kombe la dunia mwaka 2018 na
2022.
FIFA watafanya mkutano saa saba
tano asubuhi kwa saa za Uswizi (kwetu saa 7 mchana) kuzungumzia tukio
hilo na inasemekana wanapanga kuahirisha uchaguzi wa ijumaa.
Chapisha Maoni