Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


 
Ligi ya Premier Uingereza huenda itawaza bingwa wake musimu huu ikiwa vingozi Chelsea watafanikiwa kuwanyorosha wageni wao Crystal Palace uwanjani mwao Stamford Bridge Jumatatu.
Imekuwa ni hayawi, hayawi kwa Chelsea majuma kadhaa yaliopita baada ya vijana wa Jose Mourinho kuhifadhi pengo kubwa kati yao na washindani wa karibu, mabingwa watetezi Manchester City, Arsenal na Manchester United wanaowafuata kwenye msururu wa sasa wa shindano hilo mtawalia.
Chelsea watakabidhiwa kikombe mbele ya mashabiki wao ambao wamesubiri taji hilo kwa miaka mitano sasa ikiwa watazoa alama tatu dhidi ya wageni wanoongozwa na Alan Pardew na kuzindua sherehe za aina yake.
Waliwalaza Leicester City 3-1 Jumatano kuwaacha alama 13 mbele ya City na Arsenal kunusia utukufu ambao meneja Jose Mourinho alirejea tena misimu miwili iliyopita kulinyakua tena.
“Ni jambo la kifahari na furaha kuu kushinda taji lakini kulipokea nyumbani kunaongeza uhondo zaidi,” kipa mkongwe Petr Cech, alifafanua.
Kwingineko, City ambao walishindwa kumudu kasi ya Chelsea na kuanguka hadi nafasi ya nne kabla ya kujiinua tena kwa kushinda mara mbili mfululizo watatembelea Tottenham Hotspur Jumapili katika kibarua kigumu ambacho huenda hawatakuwa mabingwa tena.
Arsenal nao watajitupa uwanjani Jumatatu na Hull City ambao wanaingia mechi yao ya pili mfuatilia nyumbani na mchangamko wa kuwalaza miamba Liverpool 1-0 katikati mwa juma.
Manchester United watawania kukomesha mkimbio wa kusalimu amri mechi mbili mfululizo watakapowapokea West Brom ugani mwao Old Trafford Jumamosi wakitafuta ushindi utakaowashinikiza City na Arsenal katika vita vyao vya kumaliza nafasi ya juu zaidi.
Washika mkia Burnley ambao wanaketi alama tano kutoka usalama wataanza kuaga rasmi ligi Premier ikiwa hawatafanikiwa kushinda ugenini West Ham United.
Ratiba
Jumamosi (Zote 1400 GMT isipokuwa palipoandikwa):
Aston Villa v Everton, Leicester City v Newcastle United (1145 GMT), Liverpool v Queens Park Rangers, Manchester United v West Bromwich Albion (1630 GMT), Sunderland v Southampton, Swansea City v Stoke City, West Ham United v Burnley


Chapisha Maoni