Bondia
Francis Cheka (kushoto) akipambana na bondia Kiatchai Singwancha,
kutoka China katika pambano lao lililokuwa na raundi 10, lililochezwa
jana usiku kwenye ukumbi wa PTA Sabasaba jijini Dar es Salaam. Katika
pambanohilo, Cheka alishinda kwa KO katika raundi ya saba.
Cheka
jana alipanda ulingoni katika pambano lake la kwanza na kwa mara ya
kwanza tangu alipohukumiwa kwenda jela kwa kumpiga aliyekuwa mfanyakazi
wake huko mjini Morogoro na baadaye kupewa kifungo cha nje, ambacho bado
anakitumikia hadi sasa.
Cheka akiendelea kumuadabisha Mchina huyo,aliyeonekana kuzidiwa muda wote, huku akipiga ngumi za kushitukiza.
Mchina
akikubali yaishe kwa kukaa chini baada ya kupokea masumbwi ya kutosha
na ya maana kutoka kwa mnyama Cheka aliyekuwa na hasira na mchezo huo
ambao hajacheza tangu alipopatwa na matatizo ya kwenda jela.
Cheka
akitangazwa mshindi mwisho wa raundi ya saba na mwanzo wa raundi ya
nane, baada ya Mchina huyo kukubali yaishe mwenyeeeeeeewe, alipoamua
kukaa chini alipozidiwa.
Chapisha Maoni