Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.






KIUNGO mwenye kasi wa Yanga, Simon Happygod Msuva anaendelea vizuri na majaribio katika Klabu ya Bidvest Wits ya Afrika Kusini  timu ambayo inayomilikiwa na kitengo cha michezo cha moja ya vyuo vikuu vikongwe kabisa barani Afrika cha Wits.

Na amwesema kuwa uwezekano wa kumsajili ni mkubwa.

Wakati huo huo mchezaji  Dan Mrwanda amepata ofa ya kwenda kukipiga nchini Thailand.

Mtu wa karibu na nyota huyo amesema kuwa, Mrwanda anataka kuwaandikia barua Yanga akitaka aachwe punde tu baada ya ligi kumalizika ili awahi dirisha la usajili nchini humo.

Chanzo hicho kimesema iwapo viongozi watamgomea kutokana na kuwa na mkataba, atakubali yaishe lakini ndoto yake ni kusaka changamoto kwingine. Alisaini mwaka mmoja akitokea Polisi Moro.



Chapisha Maoni