Nikiwa kama mchezaji waki
TANZANIA ninaecheza ligi ya hapa nyumbani na nikiwa mmoja wa wachezaji katika
Timu ya Taifa ya kizazi hiki cha sasa wa Mudamrefu. Naandika hivi nikiwa na
huzuni na masikitiko makubwa juu ya mpira wetu wa TANZANIA kwa ujumla kuanzia club
zetu, ligi yetu na mpaka kwenye Timu ya TAIFA ‘TAIFA STARS’.
Sijaandika ivi kwania ya kufundisha wala kukosoa MSHABIKI, KIONGOZI WA
MPIRA, VILABU VYA TANZANIA, SHIRIKISHO LA MPIRA WA TANZANIA na wala TIMU YETU
YA TAIFA YA MPIRA WA MIGUU. Toka nilipopata akili ya kuutambua mpira wa
TANZANIA
kwakuusikiliza kwenye redio
na pia kuona bahazi ya mechi kwenye Tv za vilabu pamoja na Timu ya TAIFA
nilikuta ukiwa na lawama upande wa Wachezaji pamoja na Uongozi wa uendeshaji wa
mpira wa VILABU pamoja na TIMU YA TAIFA mpaka nilisikia timu yetu ya TAIFA IKIITWA KICHWA CHA MWENDAWAZIMU. Mimi nikiwa
kama Mtanzania pia nikiwa miongoni mwanafamilia ya mpira wa tanzania pia
inaniuma sana nikiiona mioyo ya watanzania wa penda soka mamilioni ikiteseka
kutopata furaha ya mpira.
Wewe kama mtanzania mpenda soka, Unahisi furaha inakoseshwa na
Wachezaji wa kitanzania, Uongozi na uendeshaji mpira wa kitanzani, Mashabiki wa
kitanzania au TATIZO NI NINI?????????
Kwafikra zangu mimi nahisi mpira wa tanzania unaasiriwa 1. Kutokuwa na
program za kuendesha mpira kisasa 2. Kutokuwa na misingi endelevu ya kuendesha
wachezaji wa dogo kisasa 3.kutokua na ligi kuu bora nchini 4.Kuwa na huaba wa
wachezaji wachache wanachezesha njee ya nchi ndani ya Timu ya TAIFA
5.Kutothamini na kueshimu wachezaji wakitanzania walio ndani ya ligi yetu na
njee ya ligi yetu etc.
1.
PROGRAM ZA KISASA ZA KUENDESHA MPIRA WETU.
Tanzania tupo nyuma sana yani
tunaongoza mpira kizamani sana kwa upeo wangu mimi wa sasa mpira hauchezwi na
kipaji tu Bali pamoja na elimu ya mpira Ndio manawenzetu wanakuwa na shule za
mpira, mfano’ sisi watanzania tunaleta makocha wa kisasa kwenye club zetu
pamoja na timu yetu ya taifa, ila mnasahau kuwa wachezaji wenu hawajaandaliwa
kisasa pia hata makocha wanaowafundisha sio wa kisasa. Tunatakiwa sasa tuamke
kuwapeleka makocha wetu wakajue mpira wakisasa unavofundishwa ili waje
kuwafundisha wachezaji mpira huo ili hata tukileta makocha wakigeni ambao ni
wakisasa wawe wanatuongezea kipya sio kuanza tena moja. Pia na shirikisho la
mpira liongoze mpira kisasa hata kwakuiga basi nchi zilizoendelea zaidi yetu
kimiprira kuwa walianzaje na wamewezaje sio kwa mifumo yetu hii yakizamani na
mawazo yetu ya mtu mmoja mmoja.
2.
KUTOKUWA NA MISINGI ENDELEVU YA KUENDESHA WACHEZAJI WA DOGO KISASA.
Tanzania tunauhaba wa vituo
vya kuendesha soka na kutengeneza vipaji vya vijana wadogo pia tuna utamaduni
ambao sio wakisasa wa kuinua na kutengeneza vipaji hapa nchini, sisi watanzania
club na shirikisho letu huwa wanainua vipaji sio kutengeneza vipaji kama kwa nchi
za wenzetu. Kutengeneza kipaji ni nini ?? Kutengeneza kipaji katika soka
nikumchukua Mtoto asiejua hata maana ya kupiga pasi, krosi shuti na kuanza
kumfundisha moja baada ya moja mpaka kufikia kugeuka na mpira na kupiga chenga.
Kuinua kipaji ni nini?? Kuinua kipaji nikumkuta Mtoto wa umri wamiaka 15,16
mpaka 17 na kuendelea akiwa anajua nn maana ya kupiga pasi,krosi,kugeuka na
mpira na mpaka kupiga chenga, kwamaana hiyo sasa ukifatilia club zetu hata
shirikisho letu la mpira hawana malengo na watoto wenye umri wa miaka
8,9,10,11,12,13,14 na 15 kuwaandaa ambao hawa unaweza kuwapa msingi wowote wa
soka unaoutaka Bali tunaanza na watoto wa umri wa miaka 17,18,19 na 20 na
kuendelea ambao washapitia kwenye misingi ya kizamani ambayo yamitaani ya
kupiga pasi,krosi na chenga, ambao umri huo nchi za wenzetu zilizo endelea umri
huo wa miaka 17…..20 unawakuta wakiwa tayari na wekicheza Timu kubwa pamoja na
timu ya taifa kwa mafanikio sio kwakupata uzoefu. Tuamke watanzania pamoja na
shirikisho letu na vilabu vyetu tusitake mafanikio ya haraka ambayo yanazidi
kutupotezea muda kumchukua mchezaji wa umri wa miaka 17 nakuendelea aliepitia
misingi mibovu ya mpira ndio ukataka umbadilishe na kocha wa kisasa wakigeni wa
u17 wa timu ya taifa bali tuchukue Mtoto wa miaka 8..mpaka..12 tumpe kocha wa
kisasa, madocta wakisasa, elimu ya kisasa na malezi ya soka la kisasa alfu
tuone kama hatutoweza shiriki kombe la Africa.
3.
KUTOKUWA NA LIGIKUU BORA NCHINI.
kuwa na ligikuu bora chini
nikioo kwa kuinua mpira wa nchi yetu, kwa mfano kama kwa sisi tanzania naweza
kusema asilimia 90% ya wachezaji wa Timu ya taifa wanatoka katika ligi yetu ya
nyumbani lakini kiukweli ligi yetu haina ubora kuanzia kwa maandalizi ya
wachezaji toka walipoanzia soka (mafunzo ya soka waliyoyapata) pili uendeshaji
wa club zetu hapa nchini miundombinu inayotumiwa kuendesha ligi yetu hapa
nchini mfano viwanja tunavotumia vibovu, mipira tunayotumia mibovyu kwenye ligi
jezi mbovu waamuzi sio wazuri ni waamuzi wanachezesha kizamani, kwasababu
tukija kucheza mechi zakimataifa tunakutana na mipira mizuri viwanja vizuri
waamuzi wazuri wakisasa na ndio mana timu za tanzania kwenye mashinda ya
kimataifa tunapata kadi nyingi ofsaidi nyingi mwisho tunafungwa kumbe tatizo
tulizoeshwa vibaya na marefa wa ligi yetu. Kwamaana iyo basi huwezi kumpata
mchezaji wa Timu ya taifa mzuri kutoka kwenyeligi yetu mbovu isiyo na viwanja
bora mipira bora uongozi bora marefa bora wala mashabiki bora, hiyo
nichangamoto kwetu watanzania wote wapenda soka tushtuke na tubadilike ili
mpira wetu uinuke bilaivo mtalaumu wachezaji tu mpaka Somalia watashiriki world
cup sisi hata Afican cup hatutagusa.
Waandishi
wa habari na mashabiki wa MPIRA WA TANZANIA muamke na mbadilike kunavitu
muhimu sana vya kusema ili soka la tanzania libadilike kunavitu Vingi sana vya
kusema ili vibadilishwe ili tanzania tusiwe tena vipofu kwenye ulimwengu huu wa
soka la kisasa sio soka la mdomoni wala magazetini sio soka lakupanga Timu ya
TAIFA kwenye gazeti au kwenye vijiwe jioni tukikaa ila imefikia wakati wa
kupanga timu au kuchagua timu kwa mtu husika sio kwamawazo ya mtu mmoja mmoja,
kwakufanya mabadiliko ya kuwa na ligi bora ili tupate wachezaji bora kwa ubora
wao utatengeneza Timu ya taifa bora na tutapata wachezaji wengi watakao fikia
kiwango chakucheza mpaka njee ya nchi ambao tukifikia hatua hiyo tutakua na
Timu ya TAIFA bora zaidi kwa badae ambayo tukija kupangwa tena na NIGERIA miaka
ya badae tutakua na uwakika wakuwafunga ila kwa hivi tunavoenda hatatukiwafunga
tumewabahatisha tu kiukweli TANZANIA tulipo sasa na soka la ulimwenguhuu
lilivofikia bado sana. Tubadilikeni watanzania hii niaibu si kwa wachezaji tu
ila ni kwanchi nzima mtawalaumu wachezaji tu ila wachezaji sio tatizo tatizo
tunamifumo ya kizamani alafu bado tunailazimisha iendelee.
TULISHAFELI..TUMEFELI..NA
TUSIPOAMKA TUTAFELI KABISA yani tutakua wa mwisho KABISA duniani. Ebu
jiulize wewe mwenyewe uliviona vizazi vingapi tanzania vilivyopita na vilikua
na wachezaji wazuri????? Ukipata jibu jiulize tena vilietea mafanikiogani
kwenye timu ya taifa au vilabu vyetu ambayo tunajivunia sasa???? Kwa mimi toka
nivisikie na kuadisiwa mpaka leo nacheza sijao mafanikio zaidi ya kuwa na sifa
zisizofaidisha nchi. Tubadilikeni jamani hayo nimawazo yangu tu kama
nimewakosea nisameeni ila hata sisi wachezaji mnaotutukana mais kutuona sio
wazalendo inatuumapia kwasababu tunatumia nguvu zetu bilamafanikio nakinachouma
zaidi hatupendi kufeli ila tunafelishwa inauma kwa kweli ila nyumbani ni
nyumbani TUNAIPENDA NCHI YETU NA TUTAIPENDA MILELE ila tusikubali kupelekwa tubadilikeni
watanzania
Makala
hii imeandikwa na nahodha wa Taifa Stars kwenye michuano ya Cosafa, John
Raphael Bocco
Chapisha Maoni