Timu ya taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' kesho Jumatano inatarajiwa kusafiri kuelekea
nchini Afrika Kusini kwa ajili ya kushiriki michuano ya kombe la COSAFA.
Michuano
ya COSAFA inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Mei 17 mpaka Mei 30, 2015 katika
viwanja vya Olympia Park na Moruleng jimbo la North West Province nchini
Afrika Kusini ikishirikisha nchi za Kusini mwa Afrika huku Tanzania na Ghana
zikiwa ni nchi waalikwa.
Taifa
Stars itaondoka jijini Dar es salaam kesho majira ya saa 1 jioni, kwa usafiri
wa shirika la ndege la Fasjet na kufika jijini Johanesburg saa 5 usiku.
Mara baada
ya kupimwa afya jana na madaktari wachezaji Aishi Manula, Isihaka Hassan,
Haroun Chanongo, Kelvin Friday na nahodha Nadir Haroub wamekutwa na majeruhi
ambayo yamepelekea kutokuwepo katika kikosi kitakachosafiri kesho, watabakia
nchini wakiendelea kufanya mazoezi chini ya ungalizi mpaka timu itakaporejea
kutoka Afrika Kusini na kuungana kwa ajili ya maandalizi ya AFCON, huku Amri
kiemba akipewa ruhusa kutokana na kuwa na matatizo ya kifamilia.
Msafara wa
Taifa Stars utaongozwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ephaphra Swai
ukijumuisha wachezaji 20 na benchi la ufundi, timu inatarajiwa kufikia katika
hoteli ya Sun City iliyopo pembeni kidogo ya jiji la Rusterburg.
Kesho siku
ya Alhamis kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 7 mchana ni muda wa mapumziko,
waandishi wa habari mnakaribishwa katika kambi ya timu ya Taifa iliyopo Tansoma
Hotel kuweza kuongea na wachezaji, kocha mkuu na daktari wa timu kabla ya
kuanza safari jioni.
Chapisha Maoni