BAADA ya kikao cha kamati ya
utendaji ya Simba kilichofanyika jana, Rais wa klabu hiyo, Evans Elieza
Aveva amesema Wekundu wa Msimbazi hawawezi kukaa kikao na kiungo wake
mshambuliaji , Ramadhan Yahya Singano ‘Messi’ kama ilivyoshauriwa na
TFF kwasababu
Taarifa ya Eveva iliyotumwa kwa vyombo vya habari mchana huu inasema:
“Kwa
kuwa mchezaji Ramadhan Yahya Singano alivunja makubaliano yaliyoamriwa
katika kikao cha pamoja kati ya klabu ya Simba, mchezaji mwenyewe,
SPUTANZA na Sekretarieti ya TFF, kutozungumzia yaliyojadiliwa na
kupendekezwa kwenye kikao, kwa kuyazungumza kwenye vyombo vya habari kwa
kusema yeye ni mchezaji huru, klabu ya Simba imeamua kutokufanya
mazungumzo na mchezaji huyo kwa sasa, kwa kuwa bado ina mkataba naye
ambao utaisha Julai 1 mwaka 2016.
“Ni matarajio yetu mchezaji Singano ataheshimu maamuzi hayo na mkataba ambao pia upo TFF na kwenye mtandao TMS.
Juzi uongozi wa Shirikisho la
Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) ulikutana na Uongozi wa klabu ya Simba SC
ukiwakilishwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji Collin Frisch na mchezaji
Ramadhani Yahya Singano akiandamana na Uongozi wa Chama cha Wacheaji wa
Mpira wa Miguu (SPUTANZA). Kikao hiki kiliitishwa na TFF kujadili utata
wa kimtakabta kati ya mchezaji na klabu ya Simba.
Katika kikao hicho, pande zote
zilieleza kutambua utata ulio ndani ya mikataba iliyokuwepo ambayo
kimsingi iliingiwa kabla ya uongozi wa sasa wa Simba SC.
Kwa pamoja pande hizo mbili
zilikubaliana kuanza mazungumzo ya makubaliano mapya na hatimaye mkataba
mpya utakaoanza katika msimu mpya wa 2015/16.
TFF ilivitaka vilabu kushirikiana
na SPUTANZA na Bodi ya Ligi katika kuweka mifumo mizuri ya uingiaji
mikataba. TFF inao mkataba mama (template) ambao vilabu vyote na
wachezaji wanatakiwa waufuate wakati wanaandaa mikataba yao (individual
contracts between players and clubs). Aidha TFF imewataka wachezaji
kuelewa mikataba kabla ya kutia sahihi.
TFF itazidi kuboresha mfumo wa
usajili wa wachezaji na mikataba ili kuweka mazingira sawia kati ya
pande zote mbili (Wachezaji na vilabu)
Makubaliano yaliyofanyika juzi tarehe 9 Juni 2015 yalisainiwa na:-
Collin Frisch – Simba SC
Ramadhan Singano – Mchezaji
Mussa M. Kissoky – SPUTANZA
Mwesigwa J. Selestine – Katibu Mkuu – TFF
Chapisha Maoni