Simon Msuva ameibuka kidedea
baada ya kunyakua tuzo ya mchezaji bora wa msimu wa 2014-2015
zilizotolewa na wadhamini wa ligi hiyo kampuni ya simu za mkononi ya
Vodacom na kukabidhiwa na mgeni rasmi Naibu Waziri wa Habari, Vijana
Utamaduni na Michezo Juma Nkamia kwenye hafla iliyofanyika usiku wa leo
kwenye ukumbi wa JB Belmonte (Kilimanjaro) uliopo katika jengo la Golden
Jubilee Tower (PSPF) jijini Dar es Salaam.
Msuva ambaye amechukua tuzo mbili
usiku wa leo, mbali na kuwa mchezaji bora Msuva amepewa tuzo ya
mfungaji bora baada ya kutupia kambani jumla ya magoli 17 kwenye msimu
uliomalizika Mei 9 mwaka huu na magoli hayo yaliisaidia Yanga kuibuka
mabingwa wa ligi hiyo.
Lakikini kutokana na Msuva kuwa
kwenye majukumu ya timu ya Taifa ‘Taifa Stars’, zawadi zake
zilichukuliwa na wawakilishi wake ambaye ni baba yake mzee Msuva aliye
ambana na mkewe mama yake Simon Msuva.
Msuva amewabwaga Mrisho Ngassa na Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ kwenye kinyang’anyiro hicho cha mchezaji bora wa ligi.
Nafasi nyingine ambazo zilikuwa
zikiwaniwa ni pamoja na mlinda mlango bora ambapo tuzo hiyo imenyakuliwa
na Shaban Kado (Coastal union) ambaye kwa sasa amesaini kuitumikia
klabu ya Mwadui FC ya Shinyanga akiwabwaga Mohamed Yusuph (Tanzania
Prisons) na Said Mohamed (Mtibwa Sugar).
Tuzo ya kocha bora imekwenda kwa
Mbwana Makata aliyekinusuru kikosi cha Tanzania Prisons kisishuke
daraja. Nafasi hiyo ilikuwa ikiwaniwa na Goran Kopunovic (Simba SC)
pamoja na Hans Van Der Pluijm (Young Africans).
Israel Mjuni Nkongo amenyakua tuzo ya mwamuzi bora akiwabwaga Jonesia Rukyaa na Samwel Mpenzu kwenye nafasi hiyo.
Mtibwa Sugar nao wamechukua tuzo ya timu yenye nidhamu iliyokuwa ikiwaniwa na Mgambo JKT pamoja na Wekundu wa Msimbazi Simba.
Chapisha Maoni