Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.





Na Alex Mapunda,Iringa
MAJI MAJI ya songea inatarajia kuingia kambini mapema mwenzi ujao ili kujiwinda na mshike mshike wa ligi kuu ya Vodacom msimu ujao.
Akizungumza na chanzo cha Gazeti hili Meneja wa timu God Mvura alisema hadi kufikia hivi sasa wameshasajili wachezaji 20 na bado wachezaji wanne ili kukamirisha idadi ya wachezaji ambayo  walipanga kusajili tayari kwa ligi kuu.

“Tumefikia Pazuri mwenzi ujao wiki mbili toka sasa tutaingia kambini,lengo letu ni lile lile kuchukua ubingwa wa ligi kuu na kurudisha heshima ya Maji Maji iliyopotea muda mrefu”alisema Mvula.

Aidha Uongozi wa timu ya Maji Maji Songea kwa kushirikiana na chama cha soka Manispaa,Mkoa,wadau pamoja na Mmiriki wa uwanja  chama cha Mapinduzi [CCM] wameanza kukarabati uwanja  wa Maji Maji ili kuepuka TFF kufungia uwanja huo.

uwanja huo ambao timu ya maji  maji itautumia katika ligi kuu ya vodacom Msimu ujao,wameanza kufanyia matengenezo katika pitchi ya kuchezea kwa kuotesha Nyasi Mpya,kutengeneza viti vya kisasa vya kukalia katika mabechi ya ufundi,kusafisha vyumba vya kubadilishia nguo,vyoo pamoja na uwanja wote kwa ujumla.


Chapisha Maoni