Timu
ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
Premium Lager, imewasili leo asubuhi Visiwani Zanzibar tayari kwa
maandalizi ya mchezo wa siku ya jumamosi dhidi ya timu ya Uganda kuwania
kufuzu kwa CHAN 2016.
Msafara
wa Taifa Stars unajumuisha wachezaji 21 na benchi la ufundi 7 ambao
wamefikia katika hoteli ya Nungwi Inn, mchezo dhidi ya Uganda utachezwa
katika uwanja wa Amani kisiwani Zanzibar jumamosi kuanzia majira ya saa 2
usiku.
Stars
inakutana na Uganda katika mchezo huo wa awali wa kuwania kufuzu kwa
fainali za mataifa Afrika kwa wachezaji wa ndani (CHAN) zitakazofanyika
mwakani nchini Rwanda, kabla ya kurudiana wiki mbili baadae katika
uwanja wa Namboole jijini Kampala.
Mara
baada ya kurejea kutoka nchini Misri kikosi cha Stars kiliendelea na
kambi katika hoteli ya Tansoma na kufanya mazoezi katika uwanja wa
Karume kabla ya kuondoka leo asubuhi kuelekea visiwani Zanzibar.
Kocha
mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij amewaongeza wachezaji watano ambao
hawakua katika kikosi kilichocheza dhidi ya Misri, kufuatia wachezaji wa
kimataifa wa Tanzania kutoruhusiwa kucheza mchezo huo wa CHAN wikiendi
hii.
Wachezaji
waliongezwa ni Atupele Green, Hassan Isihaka, Hassan Dilunga, Rashid
Mandawa na Kelvin Friday, wanaungana na wachezaji Deogratias Munish,
Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Oscar Joshua, Salum Mbonde, Aggrey Morris
na Nadir Haroub.
Wengine
ni Jonas Mkude, Erasto Nyoni, Mwinyi Haji, Abdi Banda, Frank Domayo,
Amri Kiemba, Said Ndemla, Saimon Msuva, na John Bocco.
Aidha
Shirikisho la Mpirani wa Miguu barani Afrika (CAF) limetoa mwongozo
kuwa mchezaji Mrisho Halfan Ngasa haruhusiwi kucheza CHAN kwa sababu sio
mchezaji tena wa ndani, hivyo Ngasa ameondolewa kikosini
Waaamuzi
wa mchezo huo wanatarajiwa kuwasili kesho kutoka nchini ambao ni Hudu
Munyemana (Rwanda), akisaidiwa na Hakizimana Ambroise (Rwanda), Justin
Karangwa (Rwanda), mwamuzi wa akiba ni Issa Kagabo (Rwanda), na
kamishina wa mchezo Nicholaus Musonye kutoka Kenya.
U15 KUINGIA KAMBINI JUMATATU
Kikosi
cha timu ya Taifa ya vijana umri chini ya miaka 15 (U-15) kitaingia
kambini siku ya jumatatu tarehe 22/06/2015 ili kujiandaa na mchezo wa
kirafiki dhidi ya kombaini ya mkoa wa Mbeya, mchezo utakaofanyika mjini
Mbeya jumatatu ya tarehe 28/06/2015.
Kikosi
hiki kinaandaliwa kwa ajili ya kujiandaa na na michuano ya mtoano
kuwania kufuzu kwa fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya
miaka 17 zitakazofanyia nchini Madagascar mwaka 2017. Hatua ya mtoano wa
awali itaanza mwakani 2016 mwezi Juni.
Timu
itakua chini ya kocha Bakari Shime kwa muda akisaidiwa na Peter
Manyika. Kocha aliyekua ameteuliwa awali kufundisha timu hiyo Adolf
Rishard ameomba udhuru baada ya kupata fursa ya kwenda masomoni.
Wachezaji
watakaoingia kambini na mikoa wanayotokea kwenye mabano ni Mwijuma
Yahya (Tanga), David Mpakazi, Shilole Anthony (Geita), Kibwana Shomari ,
Ibrahim Koba, (Morogoro), Faraji John, Kelvin Deogratius, Davison Meddy
, Maulid Lembe (Dodoma), Ally Msengi (Mwanza).
Wengine
ni Timoth Timothy, Juma Juma, Pius Raphael, Mohamed Ally (Dodoma),
Athumani Rajabu, Juma Zubeir, Jonathan Rafael (Kigoma), Robert Philip,
Jaffari Juma (Arusha), Michael Kanuti, Alex Peter, Rashid Kilongola
(Kinondoni), Morris Michael (Ilala), Karim Mfaume (Lindi), Assad Juma
(Unguja Magharibi), Francis Mrope, Kelvin Pius (Mara)
Chapisha Maoni