Klabu ya Simba sasa mambo yao safi
baada ya fedha Sh milioni 220 kuingia katika akaunti yao.
Fedha hizo ni malipo ya mauzo ya
mshambuliaji Emmanuel Okwi Arnold kwenda katika klabu ya Sonderjyske ya nchini nchini Denmark.
Sonderjyske
ilikubali kulipa dola 110,000 ili kumnasa Okwi. Ikaahidi kulipa fedha hizo Juni
17 na imechelewa kidogo tu lakini imeweza kutimiza ilichoahidi.
Habari
za uhakika kutoka Simba, zimeeleza kuwa Sonderjyske imeilipa Simba kupitia
akaunti yake ya CRDB jijini Dar es Salaam.
Mshambuliaji Emmanuel Okwi
ambaye uhamisho wake daima umekuwa ukizungukwa na maswali kila aendako,
ameingia katika utata mwingine baada ya ripoti mpya kudai kwamba
alisaini mkataba wa miaka mitano wa kuichezea timu ya SønderjyskE licha
ya timu hiyo ya Denmark kutotoa hata senti kwa klabu yake ya Simba.
Utata huo mpya umefuatia
Wadenmark hao kutaka kumrejesha Okwi Simba kwa mkopo wa miezi sita baada
ya kukwama kuipata leseni yake ya uhamisho ya kimataifa (ITC), ambayo
Simba imesema haitaitoa hadi itakapolipwa ada ya uhamisho dola 110,000
(sawa na Sh. milioni 220).
Kumekuwa na mitazamo kwamba
kutolewa kwa mkopo kwa Okwi Simba kunaweza kuwa ni janja ya timu hiyo ya
Denmark kuvizia Mganda huyo amalize mkataba wake Msimbazi unaomalizika
Mei mwakani ili imchukue bure.
Hata hivyo, klabu kubwa kama ya
Simba inatarajiwa kwamba ilisaini mkataba na SønderjyskE ambao
unaifunga klabu hiyo ya Ligi Kuu ya Denmark kwamba lazima ilipe deni
hilo, hata kama itamleta Msimbazi kwa mkopo.
Taarifa nyingine zinasema kuwa
klabu hiyo ya Denmark imefikia uamuzi huo baada ya kumnasa mchezaji
mwenye kiwango cha juu zaidi ukilinganisha na Okwi na gharama zake za
usajili ni za chini.
Rais wa Simba, Evans Aveva,
alisema kwamba kwa sasa wao wanachofuatilia ni kuhakikisha wanalipwa
kiasi hicho cha fedha ndipo waruhusu usajili wa njia ya mtandao
ufanyike.
Aveva aliweka wazi kwamba,
walimuuza Okwi baada ya mchezaji kuangalia maslahi yake na sasa umefika
wakati klabu kuhakikisha inapata haki yake na si kuona makosa
yaliyofanyika huko nyuma yanajirudia.
Katika uongozi wa Mwenyekiti,
Ismail Aden Rage, Okwi aliuzwa kwa klabu ya Etoile du Sahel kwa dau la
Dola za Marekani 300,000 lakini fedha hizo hazikulipwa hadi leo na
baadaye mshambuliaji huyo alirejea klabu yake ya zamani ya SC Villa na
muda mfupi alijiunga na Yanga.
Mganda huyo aliichezea Yanga
katika kipindi kifupi na kurejea Simba kwa kueleza kuwa mabingwa hao wa
Tanzania Bara hawakutimiza baadhi ya vipengele vilivyoko kwenye mkataba
wake.
ILA KWA SASA SIMBA WAMESHAPATA PESA ZAO.
Chapisha Maoni