Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


klabu-ya-simba1-768x403
Klabu ya Simba kwa kushirikiana na Jumia wamezindua huduma ya kununua jezi za Simba za 2015 – 2016 kupitia duka la mtandao la Jumia www.jumia.co.tz . Dhumuni la huduma hii ni kuwapatia wapenzi wa klabu ya Simba njia bora ya kuweza kununua jezi popote walipo Tanzania.

Kupitia mtandao imara na wenye uzoefu wa Jumia, klabu ya Simba inapanga kuongeza upatikanaji wa vifaa vyake vya michezo nchi nzima.Mkataba huu utatanua wigo wa usambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu ya Simba. “Kwa kuzingatia upana wa upatikanaji wa huduma za mtandao, 

klabu ya Simba inafahamu umuhimu wa kuvifanya vifaa vyake vya michezo kuweza kupatikana kiurahisi kwa wapenzi wake popote walipo Tanzania, hivyo leo tunajivunia kuzindua uzindizi wa duka la mtandao Jumia – Simba Online Shop kwa ajili ya kutumia mtandao wa Jumia kuwezesha wapenzi wa Simba popote walipo kuweza kununua mavazi na bidhaa za Simba kiurahisi na kwa bei nafuu”. Alisema Rais wa Simba Evans Aveva.

Maneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul aliongeza kwa kusema “uzinduzi wa jezi za mpira wa miguu mara zote ni tukio muhimu kwenye maisha ya klabu maarufu na inayopendwa kama Simba. 

Katika msimu wa 2015 – 2016 klabu ya Simba imeamua kuwa wabunifu kwa kutoa fursa kwa wapenzi wake kununua jezi za msimu 2015 – 2016 kupitia njia ya mtandao. 

Tunajivunia sana kwa klabu ya Simba kutuchagua Jumia kwa kazi hii. Kupitia huu umoja wetu wa Simba na Jumia tumeamua kutoa ofa kwa wanachama na wapenzi wa Simba kuagiza jezi kuanzia Jumatatu tarehe 27 – 7 – 2015 mpaka Alhamisi 31 – 7 – 2015 kupitia www.jumia.co.tz kabla ya kuanza rasmi kwa mauzo ya kimtandao kupitia Jumia na kuanza kuuzwa rasmi kwa rejareja”.

“Tunawahamasisha wapenzi wa Simba popote walipo Tanzania kuagiza jezi kupitia www.jumia.co.tz na kufurahia urahisi katika kufanya manunuzi. 

Popote walipo wapenzi wa Simba wanaweza kuagiza jezi kupitia tovuti ya jumia na kuletewa mizigo yao mpaka mlangoni. Jumia pia inatoa njia tofauti za ulipia kama vile kulipia pindi mzigo wako utakapofika au kufanya malipo kupitia simu za mkononi. Kuanzia jumatatu 27 – 7 – 2015 wapenzi wa Simba watapata fursa ya kuagiza jezi kupitia www.jumia.co.tz”. Aliongeza Meneja wa Jumia nchini Tanzania Jean –Philippe Boul.

Kuzungumzia mapinduzi haya makubwa katika usambazaji wa vifaa vya michezo vya klabu ya Simba, Mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya EAG group Limited Imani Kajula ambao ni washauri na watekelezaji wa masuala ya kibiashara na masoko ya klabu ya Simba alisema “mapinduzi haya makubwa yataiwezesha klabu ya Simba kuongeza mapato yake na pia kudhibiti bidhaa za kughushi, kupitia Jumia Online Shop (duka mtandao la Jumia) wapenzi wa Simba watanunua bidhaa za Simba kupitia washirika halali wa uuzaji wa bidhaa za Simba Tanzania. Katika siku chache zijazo tutaeleza wapenzi wa Simba maduka ya rejareja ytakayo kuwa yanauza jezi za Simba 2015 – 2016.”


Chapisha Maoni