Hatua ya nusu Fainali ya Michuano ya Kombe la Vilabu Bingwa Afrika
Mashariki na Kati (Kagame Cup) inatarajiwa kuendelea kesho katika uwanja
wa Taifa, huku kiingilio cha chini katika michezo hiyo kikiwa ni
shilingi elfu tatu (3,000).
Viingilio vingine vya michezo hiyo ya kesho ni VIP A ni shilingi
elfu kuni na tano (15,000) na VIP B & C, Shilingi elfu kumi (10,000)
na sehemu nyingine ya uwanja iliyobakia ni shilingi elfu tatu (3,000)
kwa viti vya rangi ya bluu, kijani na rangi ya chungwa.
Timu nne kutoka katika nchi nne wanachama wa michuano hiyo, Azam FC
(Tanzania), Gor Mahia (Kenya), KCCA (Uganda) na Al Khartoum (Sudan)
zimefuzu kwa hatua ya nusu fainali itayochezwa uwanja wa Taifa siku ya
ijumaa.
Mchezo wa kwanza utakaonza saa 7:30 mchana utazikutanisha timu za
Gor Mahia ya Kenya itakayocheza dhidi ya Khartoum ya Sudan, mchezo
unaotarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kufutia timu hizo kutoka sare katika
mchezo wake wa awali hatua ya makundi.
Katika mchezo wa kwanza uliozikutanisha timu hizo, kocha wa
Khartoum Kwesi Appiah na Frank Nuttal wa Gor Mahia walitoka sare ya bao
1- 1 ndani ya dakika 90, hali ambayo inapelekea kufaya mchezow wa kesho
kuwa mgumu kwa kila timu kuhitaji nafasi ya kusonga mbele hatua ya
fainali.
Gor Mahia mabingwa mara tano wa michuano hiyo, wataingia uwanjani
kusaka ushindi ili kusonga hatua ya fainali ili waweza kutwaa ubingwa
huo kwa mara ya sita, sawa na klabu ya Simba inayoongoza kwa kutwaa
ubingwa huo.
Kocha Frank Nuttal atakua akiwategemea wachezaji wake nyota, Khalid
Alucho, Kagere Meddie, Michael Olunga, Sibomana Abouba, Karim
Nzigiyimana, Godfrey Walusimbi, Nahodha Musa Mohamed, na mlinda mlango
Boniface Oluoch katika kusaka ushindi dhidi ya Khartoum.
Kwesi Appiah atashuka dimbani akiwategemea wachezaji wake nyota,
Antony Akumu, Dominic Abdui, Samawal Meshani, Wagdi Wawd, Ouismaila Baba
na nahodha Amin Ibrahim.
Vita kali itakua kwa washambulaji Michael Olunga wa Gor Mahia na
Salaheldin Osman wote wenye mabao manne, wakiwania kuongeza bao katika
mchezo huo wa kesho ili kujiweka katika mazingira mazuri ya kutwaa kiatu
cha dhahabu.
Nusu fainali ya pili itawakutanisha waoka mikate wa Azam FC dhidi
ya Mamlaka ya jiji la Kampala (KCCA), mchezo utaokanza majira ya 9:45
kwa saa za Afrika na Kati katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mchezo huo pia unatarajiwa kuwa na upinzani mkali kufutia timu hizo
katika mchezo wa hatua ya makundi, Azam FC kuibuka na ushindi wa bao 1-
0, bao liliofungwa na nahodha wake John Bocco.
KCCA chini ya kocha wake Mike Mutebi watashuka dimbani kusaka
ushindi katika mchezo huo, ikiwa ni kulipiza kisasi kwa mchezo wa kwanza
na kupata ushindi utakaowavusha mpaka katika hatua ya fainali.
Kocha Mutebi atakuwa akiwategmea wachezaji wake nyota, Nahodha Tom
Matiko, Opio Emmanuel, Joseph Ochaya, Hassan Waswa, Isaac Sserenkuma,
Habib Kavuma na Muzamil Mutyaba.
Azam FC itashuka dimbani kutaka kuendeleza ubabe wake dhidi ya KCCA
ya Uganda, na kuweza kukata tiketi ya kucheza fainali siku ya jumapili
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Kocha wa Stewart Hall wa Azam atakua akijivunia safu yake ya ulinzi
ambayo haijaruhusu bao tangu kuanza kwa michuano hiyo, huku safu yake
ya ushambuliaji ikiwa imefunga mabao 8 katika michezo mine iliyocheza.
Hall atashuka dimbani akiwategema nyota wake Nahodha John Bocco,
Pascal Wawa, Aggrey Morris, Himid Mao, Kipre Tchetche, Jean Baptist
Mugiranenza, Frank Domayo na mlinda mlango Aishi Manula.
TFF YAIPONGEZA AZAM FC
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi
ametuma salam za pongezi kwa klabu ya Azam FC kwa kufanikiwa kuingia
katika hatua ya nusu fainali ya michuano ya Kombe la Kagame inayotimua
vumbi jijini Dar es salam.
Katika salamu zake kwa uongozi wa klabu ya Azam, Malinzi amewataka
kutobweteka na kuongeza bidii katika hatua hiyo ya nusu fainali ili
waweze kufuzu kwa hatua ya fainali na kutwaa Ubingwa huo na kuwaomba
watanzania wote kuwasapoti wawakilishi pekee wa nchi kwenye michuano
hiyo
TFF kwa niaba ya familia ya mpira na watanzania wote, inatwakia
kila la kheri Azam FC katika mchezo wake wa kesho wa nusu fainali dhidi
ya KCCA.
TFF YATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) limetuma salam za rambi
rambi kwa familia ya Moshi Shaban, kufutia kifo cha Moshi kilichotokea
jana jijini Dar s salaam na mazishi kufanyika leo jijini Dar es salaam.
Katika salamu zake za rambirambi kwa familia ya marehemu Moshi, TFF
imewapa pole wafiwa, ndugu jamaa na marafiki na kusema wako pamoja
katika kipindi hiki cha maombelezo na kuomba mwenyezi Mungu awajilie
nguzu wafiwa
Marehemu Moshi Shaban ni baba wa wachezaji waliowahi kuichezea timu
ya Taifa ya Tanzania, Haruna Moshi “Boban) na Iddy Moshi (Mnyamwezi).
TFF YAANDAA KOZI YA WAAMUZI WA LIGI KUU NA LIGI DARAJA LA KWANZA MSIMU WA 2015/2016
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) linaandaa kozi ya
waamuzi wa mpira wa miguu watakaochezesha mechi za Ligi Kuu na Ligi
Daraja la Kwanza 2015/2016, kozi hiyo itafanyika jijini Dar es salaam
kuanzia tarehe 21 -24/08/2015.
Washiriki wa kozi hii ni waamuzi waliochezesha mechi za Ligi Kuu na
Ligi Daraja la Kwanza msimu wa 2014/2015 wenye umri wa miaka 21 – 45
kwa wanawake na miaka 23 – 45 kwa wanaume.
Waamuzi wote wanatakiwa kuripoti tarehe 21/08/2015 katika ofisi za
TFF zilizopo Karume Ilala Dar es salaam na wawasilishe vyeti halisi vya
kuzaliwa na nakala zake.
Pamoja na cheti cha kuzaliwa kwa kila mwamuzi ni lazima alete kadi
ya kupigia kura au passport ya kusafiria kwa ajili ya uthibitisho wa
umri wake.
Washiriki wa kozi watafanya mitihani ya kupima afya, utimamu wa
mwili na sheria za mpira wa miguu Trivia (kuandika), video clips
(offside na match analysis).
Waamuzi watakaofaulu watashindanishwa kupata waamuzi arobaini (40) na
waamuzi wasaidizi sabini (70) watakaochezesha Ligi Kuu na Ligi
Daraja la Kwanza kwa msimu wa 2015/2016. Shirikisho linawatakia wote
maandalizi mema.
Baada ya kozi ya waamuzi kutakuwa na kozi ya makamisaa wa Ligi Kuu
ya Vodacom na Ligi Daraja la Kwanza ambayo itafanyika kuanzia tarehe
24/08/2015 hadi tarehe 25/08/2015.
Makamisaa wote wanatakiwa kuripoti tarehe 23/08/2015 saa 10:00
alasiri uwanja wa Taifa, Makamisaa watakao husika na kozi hii ni wale
wote walio simamia michezo ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza kwa
msimu wa 2014/15.
Makamisaa watafanya mtihani wa sheria za mpira wa miguu (Trivia,
offside, match analysis) na kupima mwamuzi anapochezesha (evaluation).
Wale watakaofaulu ndiyo watakaopangwa kusimamia michezo hiyo.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF)
Chapisha Maoni