IMEKUWA KWELI,Azam FC iumeifunga Gor Mahia kwa mabao 2-0 na kubeba ubingwa wa Kagame wakiwa hawajafungwa hata bao moja.
Mwaka 2002, Tusker ya Kenya ilifanya hivyo, lakini Azam FC imefanya hivyo huku ikiwa haijafungwa hata bao moja, Simba na Yanga hazijawahi kufanya hivyo.
Bao la kwanza la Azam FC lilifungwa na John Bocco ambaye aliipangua beki ya Gor kabla ya kupiga krosi safi kabisa iliyomfikia Bocco akamaliza kazi.
Bao la pili, likafungwa Kipre ambaye alipiga mpira wa adhabu na kipa wa Gor akadhani unatoka.
Baada ya hapo, Gor iliendelea kupambana lakini ilishindwa kuukamata mziki wa Azam FC ambao walikuwa safi huku beki Serge Wawa akimtuliza mshambuliaji hatari Michael Olunga.
Kwa ushindi huo, timu hiyo ya Alhaj Sheikh Said Salim Awadh Bakhresa na familia yake inazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani 30,000 (Sh. Milioni 60), wakati Gor Mahia wanapozwa na dola 20,000 (Sh. Miliioni 40).

Chapisha Maoni