LEO ndio rasmi Msimu mpya wa Soka huko England unafunguliwa kwa Mechi maalum ya kugombea Ngao ya Jamii kati ya Mabingwa wa England Chelsea na waliobeba FA CUP Arsena; itakayochezwa Uwanjani Wembley Jijini London.
Mtanange huu, kila Mwaka, ndio hutangulia kwa Wiki 1 kabla kuanza kwa Ligi Kuu England ambayo safari hii itaanza Wikiendi ijayo, hapo Jumamosi Agosti 8, na Mechi ya kwanza kabisa ni huko Old Trafford kati ya Manchester United na Tottenham.
Hali za Timu
Meneja wa Chelsea Jose Mourinho amethibitisha kuwa Wachezaji wake Wawili waliokuwa na maumivu Diego Costa na Beki Gary Cahill wote wako fiti kucheza.
Arsenal wao hawajaripotiwa kuwa na Majeruhi yeyote.
TAKWIMU
-Arsene Wenger hajamfunga Jose Mourinho katika Mechi 13, Sare 6 Kufungwa 7.
-Mara ya mwisho kwa Timu iliyotwaa Ngao ya Jamii na kwenda kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England Msimu huo huo ni Manchester United Mwaka 2010.
Bosi wa Arsenal, Arsene Wenger, hajawahi kuifunga Timu ya Jose Mourinho na wameshakutana mara 13 huku Wenger akiwa bado kuonja ushindi.
Hali hii imezidi kuleta uhasama kati ya Mameneja hao na kauli kati yao Siku zote zina ushindani mkubwa na maneno makali huku kila mmoja akimpiga kijembe mwenzake.
Hata hivyo, Jana Mourinho alijaribu kupooza uhasama wake na Wenger kwa kudai: "Sijali kuhusu Arsenal wala Meneja wao na wala sijisifii kuhusu ushindi wangu dhidi ya Arsenal. Sitalalamika ikiwa Siku moja tutafungwa!"
TAKWIMU
-Mara mbili za mwisho kwa Chelsea kutwaa Ngao ya Jamii, Msimu huo huo walitwaa Ubingwa-Miaka ya 2005 na 2009.
-Chelsea na Arsenal zimewahi kukutana mara moja tu kwenye Nagao ya Jamiii Mwaka 2005 na Chelsea kushinda 2-1. Bao la Arsenal kwenye Mechi hiyo lilifungwa na Cesc Fabregas ambae sasa yuko the Blues.
-Hii ni mara ya 21 kwa Arsenal kucheza Ngao ya Jamii na wameshinda mara 12, kufungwa 7 na Sare 1 wakati Chelsea ni mara ya 11 wakishinda 4 na kufungwa 6.
-Chelsea na Arsenal katika Mechi 8 wakishinda 5 Sare 3.
Chapisha Maoni