Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kwa nini John Bocco ‘Adebayor’ anatajwa kuwa ndiye mchezaji bora wa muda wote wa AzamFC?
  1. Mchezaji pekee ambaye amecheza Azam FC tangu ikiwa ligi daraja la kwanza mpaka sasa.
  2. Alifunga goli dhidi ya Majimaji na kuisaidia Azam kupanda daraja na kucheza ligi kuu kwa mara ya kwanza kwenye msimu wa 2008-2009
  3. Ameisaidia Azam kutwaa vikombe vitatu vikubwa, kombe la ligi kuu Tanzania bara mara mbili (2012 na 2014) pamoja na Kagame Cup (2015).
  4. Bocco ndiye mchezaji aliyefunga magoli mengi kuliko mchezaji yeyote kwenye timu ya Azam FC
  5. Nahodha wa kikosi cha Azam FC
Wasifu wake (John Bocco):
Jina kamili: John Raphael Bocco
Tarehe ya kuzaliwa 05/08/1989
Uraia: Mtanzania
Nafasi anayocheza: Mshambuliaji
Timu anayocheza kwa sasa: Azam FC na timu ya Taifa ya Tanzania
Urefu: sm 182
Anavaa jezi namba: 19
Leo John Bocco ‘Adebayor’ anaadhimisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwake (Agosti 5) akiwa anafikisha umri wa miaka 26.
Mtandao huu unamtakia Bocco maadhimisho mema ya siku yake ya kuzaliwa na kumuombea maisha mema na marefu katika soka na jamii kwa ujumla.
Mashabiki wa timu ya Azam FC wakiwa wameshika T-Shirt iliyoandikwa maneno ya kumsifia nahoha wa kikosi chao John Bocco 'Adebayor'
Mashabiki wa timu ya Azam FC wakiwa wameshika T-Shirt iliyoandikwa maneno ya kumsifia nahoha wa kikosi chao John Bocco ‘Adebayor’



Chapisha Maoni