Shrikisho
la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesaini mkataba mpya wa miaka mitatu
(3) wa udhamini wa ligi kuu Tanzania bara kuanzia msimu ujao na
mdhamini mkuu wa ligi hiyo ambayo ni kampuni ya simu za mkonnoni ya
Vodacom.
Katibu mkuu wa TFF Selestine
Mwesigwa amethibitisha kusainiwa kwa mkataba huo lakini akasema
hawakufanya sherehe za kutia saini mkataba huo kutokana na mashindano
ya Kagame yaliyokuwa yanaendelea nchini wakati TFF ilikuwa ikiyasimamia
kama shirikisho la soka la nchi mwenyeji.
“Kunakitu wanasema katika ajira,
unaposikia nafasi haijatangazwa na hajatangazwa mtu mpya jua kwama kuna
maendeleo na maranyingi ‘renewal’ ya ‘contract’ huwa hai-sound sana kama
tunapoongelea mkataba ambao watu wameingia udhamini mpya”, amesema
Mwesigwa.
“Bila shaka mdhami wa msimu wetu
unaokuja ni Vodacom ambae tulikuwanae msimu uliopita, kila kitu
kimeshawekwa sawa ila kwa maana ya ceremony ndio bado haijafanyika
kwasababu kulikuwa na mambo mengi hapa katikati ya Kagame na kadhalika”.
“Mkataba ni miaka mitatu,
kutakuwa na maongezeko ukizingatia kuna timu zimeongezeka lakini nadhani
hata kile kinachokwenda kwenye vilabu kitaongezeka kwa kiasi fulani
yako masuala mengi siwezi kuzungumza kwa undani kwa sasahivi, kwa upande
wa kwetu tulikuwa tunayaona hayapo sawasawa. Kulikuwa na muda mwingi
sana wakutosha kujadili karibu miezi nane iliyopita kwahiyo kuna vitu
vingi vimeangaliwa”.
Kwasababu sherehe ya kusaini
mkataba haijafanyika, sitaweza kuingia kiundani zaidi lakini ni mkataba
ulioboreshwa ukilinganisha na mikataba iliyotangulia”.
Chapisha Maoni