Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Kamati ya masaa 72 ya uendeshaji wa Ligi Kuu imepitia ripoti mbalimbali za
michezo iliyochezwa ya Ligi Kuu na Ligi Daraja la
Kwanza nchini imemfungia mchezji Juma Nyoso
wa timu ya Mbeya City kucheza mpira wa miguu
kwa kipindi cha miaka miwili na faini ya shilingi
milioni mbili (2,000,000) kufutia kitendo cha
udhalilishaji alichomfanyia mchezaji wa Azam FC
John Bocco.
Nyoso alifanya kitendo hicho katika mchezo no
namba 32 wa VPL kati ya Azam FC na Mbeya
City uliofanyika kwenye uwanja wa Chamazi, Dar
es Salaam, kutokana na kuwa tabia ya kufanya
vitendo hivyo vya utovu wa nidhamu mara kwa
mara kwenye michezo ya Ligi Kuu.
Klabu ya Young Africans imepigwa faini ya shiligi
laki tano (500,000) kufutia wachezaji wake
watano kuonyeshwa kadi za njano katika mchezo
dhidi ya Simba SC. Kwa mujibu wa kanunu
namba 42 (11) timu ambayo wachezaji wake
watapata kadi zaidi ya tabo katika mchezo
mmoja itapigwa faini ya shilingi laki tano.
Wachezaji waliopata kadi za njano wa Young
Africans katika mchezo huo ni ni Salum Telela,
Mbuyu Twite, Malimi Busungu, Ali Mustafa na
Mbuyu Twite.
Aidha klabu ya Yanga imepigwa faini nyingine ya
shilingi laki tano (500,000) kufutia wachezaji
wake kwenda kushangilia upande wa Simba SC
mara baada ya mchezo kumalizika.
Mchezo utatazamwa tena ili kuangalia
malalamiko ya Simba SC dhidi ya mwamuzi.
Simba pia inapigwa faini baada ya wapenzi na
mashabiki wa timu hiyo kuwashambulia waamuzi
baada ya mchezo ambapo waliwarushia chupa za
maji ambazo nyingine ziliwakosa waamuzi na
kumpata kocha wa Yanga Hans Van Pluijm.
Mchezo namba 26 wa VPL kati ya Coastal Union
na Mwadui uliofanyika kwenye uwanja wa
Mkwakwani, Tanga. Chumba cha Coastal Union
kilikuwa na harufu kali sana. Baadhi ya mashabiki
wa Coastal Union waliokuwa nyuma ya goli la
upande wa kaskazini walitoa lugha ya matusi
kwa waamuzi na kutishia kuwapiga na pia
walimrushia mawe mwamuzi msaidizi wa pili
Shafii Mohamed na jiwe moja lilimpiga mgongoni
na kumjeruhi kidogo mwamuzi na aliomba
msaada wa jeshi la polisi kutuliza ghasia, mchezo
ulisimama kwa dakika 3.
Kwa mujibu wa kanuni namba 42 (1) ya udhibiti
wa wachezaji Coastal Union itatozwa faini ya Tsh
500,000/=
Mchezo namba 22 wa VPL kati ya Mtibwa Sugar
na Ndanda uliofanyika kwenye uwanja wa
Manungu, Turiani. Ndanda hawakuleta watu wa
kutosha kwenye pre match meeting hivyo
wanapigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000/=)
Mchezo namba 23 wa VPL kati ya Simba SC na
Kagera Sugar uliofanyika kwenye uwanja wa
Taifa, Dar es salaam. Simba walikuwa na
wajumbe watatu na Kagera Sugar walikuwa na
mtu mmoja tu tena hakuja na vifaa. Timu zote
zimepigwa faini ya shilingi laki mbili (200,000).
Mchezo namba 17 wa VPL kati ya Stand united
na African Sports kocha wa Stand United
alitolewa nje ya eneo la ufundi kwa kutoheshimu
taratibu za eneo hilo na pia alikataa kuongea na
vyombo vya habari kwa hiyo kwa mujibu wa
kanuni namba 40 (11) anafungiwa kukaa kwenye
benchi la ufundi kwa mechi mbili na faini ya sh
500,000/= kwa kila kosa jumla 1,000,000/=.
Friends Rangers na KMC Mechi Na 8 Kundi A
iliyofanyika uwanja wa Karume 27.9.2015. Timu
ya KMC ya kinondoni ilifanya mabadiliko kwa
kuingiza wachezaji 4 ambao ni kinyume cha
kanuni. Kwa mujibu wa taarifa ya mwamuzi
wachezaji waliofanyiwa mabadiliko ni
i. Frank Mashoto badala ya Kudra Omari
ii. Kamongo Morris badala ya Mrisho Simon
iii. Mfanyeje Musa badala ya Kabange Mgunda na
iv. Sultani Kasiras badala ya Adam Said
Kwa mujibu wa kanuni namba 14 (25) KMC
imepoteza mechi na kupigwa faini ya Tsh
200,000/=. Mwamuzi wa akiba anafutwa
kuchezesha ligi msimu huu na mwamuzi wa kati
anapewa onyo.



Chapisha Maoni