VPL KUENDELEA VIWANJA SABA
Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara inatarajiwa
kuendelea leo Jumatano kwa timu 14 kucheza
katika viwanja saba nchini, ikiwa ni raundi ya
tano ya ligi hiyo iliyoanza kutimua vumbi
Septemba 12, 2015.
Simba SC watakua wenyeji wa Stand United
katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Azam
FC watawakaribisha Coastal Union kwenye
uwanja wa Azam Complex – Chamazi jijini Dar es
salaam.
Mjini Morogoro vinara wa ligi hiyo Young Africans
watakua ugenini kuwakabili wenyeji Mtibwa Sugar
ambapo timu zote zikiwa na alama 12 baada ya
kucheza michezo minne zikipishana kwa tofauti
ya magoli, Wana Lizombe Majimaji FC watakua
wenyeji wa Ndanda FC kwenye uwanja wa
Majimaji mjini Songea.
Wakata Miwa wa Kagera Sugar watawakaribisha
maafande wa JKT Ruvu katika uwanja wa Ali
Hassan Mwinyi mjini Tabora, African Sports
wakiwakaribisha wa Mgambo Shooting uwanja
wa Mkwakwani jijini Tanga, huku Tanzania
Prisons wakiwa wenyeji wa Mwadui FC katika
uwanja wa Sokoine jijini Mbeya.
Ligi hiyo ya Vodacom itaendelea siku ya Alhamis
kwa mchezo mmoja ambapo Toto Africans
watakuwa wenyeji wa Mbeya City katika uwanja
wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
IMETOLEWA NA TFF
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
Tanzania Football Federation - TFF
Asante kwa kutembelea Hope FM Iringa, Asante kwaku-share habari hii, Kama una Maoni, Ushauri, Story ya ku-share na sisi na au Unahitaji msaada...!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Wasiliana nasi kwa Email hopefmiringa@gmail.com au ungana nasi kupitia mitandao ya kijamii hapo chini!
Jisajili kwenye:
Chapisha Maoni (Atom)
Chapisha Maoni