Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


JUMAPILI Jiji la Manchester huko England leo
Linazizima kwa Dabi ya 170 kati ya Mahasimu
Manchester United na Manchester City katika
Mechi ya Ligi Kuu England.
Hadi sasa Man United ndio wanaongoza kwa
kushinda Dabi 70 huku City wakishinda 49 tu.
Msimu uliopita kwenye Mechi kama hii, ikiwa ni
Dabi ya kwanza Uwanjani Old Trafford kwa
Meneja wa Man United, Louis van Gaal, Man
United ilishinda Bao 4-2.
Safari hii, Man City, chini ya Meneja Manuel
Pellegrini, wataingia dimbani wakiwa pungufu
kwa kuwakosa Mastaa wao wakubwa Majeruhi
David Silva na Sergio Agüero.
Lakini City wanao Wachezaji wapya
waliowanunua Msimu huu, Kevin De Bruyne na
Raheem Sterling, huku Wilfried Bony akivaa
viatu vya Aguero kwa kucheza kama Straika.

DABI 3 ZILIZOPITA:
-Manchester United 4 (Young, Fellaini, Mata,
Smalling) Manchester City 2 (Aguero 2)
Ligi Kuu England, Aprili 2015
-Manchester City 1 (Aguero) Manchester United
0
Ligi Kuu England, Novemba 2014
-Manchester United 0 Manchester City 3 (Dzeko
2, Toure)
Ligi Kuu England, Machi 2014

Kama kawaida, Man United wataongozwa na
Kepteni wao Mpiganaji Wayne Rooney, ambae
ametimiza Miaka 30, akisaidiwa na Chipukizi
wao wapya Memphis Depay na Anthony Martial.
Baada ya Mechi 9 za Ligi, Man City wako
kileleni wakiwa na Pointi 21 wakifuatiwa na
Arsenal na Man United zote zikiwa na Pointi 19
huku West Ham wakishika Nafasi ya 4 wakiwa
na Pointi 17.



Chapisha Maoni