Mwenyekiti wa kamati ya Taifa Stars
Farough Baghozah (katikati) akiitambulisha kamati yake mbele ya
waandishi wa habari kushoto ni Michael Wambura-Makamu Mwenyekitina kulia
ni Bi Teddy Mapunda-Katibu
Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa Stars
iliyoteuliwa hivi karibuni na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) Bwana
Farough Baghozah leo hii amekutana na waandishi wa habari katika hoteli ya
Serena jijini Dar es salaam na kuitambulisha rasmi kamati hiyo.
Katika kamati hiyo ya Taifa ya Stars
wapo Michael Wambura – Makamu Mwenyekiti, Bi Teddy Mapunda – Katibu, Wakili
Imani Madega – Mweka Hazina, na wajumbe wengine ni Juma Pinto, Isaac Chanji,
Salum Abdalla na Moses Katabaro.
Pia Mwenyekiti amechukua fursa hiyo
kutangaza kamati ndogondogo na wajumbe wake kama ifuatavyo:
1. Maandalizi ya timu, zikiwemo
huduma kwa timu ya Taifa stars
Mwenyekiti – Imani Madega
Wajumbe – Msafiri Mgoyi,Teddy
Mapunda.
2. Uhamasishaji wa mchezo (Michezo
ijayo) na Masoko
Mwenyekiti – Juma Pinto
Wajumbe – Baraka Kizuguto, Mlamu
Ng’ambi, Charles Hamka, Hashim Lundenga, Maulid Kitenge, Shaffih Dauda,
Salehe Ally, Peter Simon, Edo Kumwembe na Mahmoud Zubeiry.
3. Kamati ya Fedha
Mwenyekiti – Farough Baghozah
Wajumbe – Teddy Mapunda, Michael
Wambura, Imani Madega,
Juma Pinto, Isaac Chanji, Moses
Katabaro na Edgar Masoud.
4. Mikakati ya ushindi – itakuwa na
kamati ndogondogo na zitakuwa na wajumbe mbalimbali wakiwemo Mwenyekiti Farough
Baghozah, Teddy Mapunda, Mohamed Nassoro, Philemon Ntahilaja, Isaac Kasanga,
Cresencius Magori.
Pia kamati imetangaza kauli mbiu ya
ushindi inayosema “NCHI YETU, TIMU YETU, TAIFA LETU, USHINDI WETU” itakayoanza
kutumika kuanzia leo hii. Pia Kamati imemteua Bi Teddy Mapunda kuwa
msemaji mkuu wa kamati hiyo.
Timu inatarajia kuweka kambi Nje ya
Nchi kwa takribani siku 12 ili kujiandaa na mechi dhidi ya Algeria Novemba 14
Dar es salaam, na Novemba 17 nchini Algeria.
Aidha Mwenyekiti alitumia nafasi
hiyo kuwaomba Watanzania wote warudishe imani kwa timu yao, wajitokeze kwa
wingi kwenye mechi ijayo tarehe 14 November dhidi ya Algeria hapa
nyumbani. Pia akatoa wito kwa Watanzania Wote kuchangia timu kwa hali na
mali (Madawa, Maji, vifaa vya michezo na kadhalika)…aliongeza ‘Mwenyekiti wa
Kamati Bwana Farough Baghouzah.
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
TFF
Chapisha Maoni