Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Mshambuliaji wa Simba,
Mganda, Hamisi Kiiza, leo
Jumatano anaweza kuukosa
mchezo wa Ligi Kuu Bara
wakati timu yake
itakapopambana na Coastal
Union kwenye Uwanja wa
Taifa, Dar kutokana na
kutokuwa fiti asilimia mia.
Kiiza ambaye bado hajapona
vizuri majeraha ya nyama za
paja, tayari ameanza
mazoezi tangu wiki
iliyopita lakini kwa
tahadhari kubwa.
Katika mazoezi ya juzi
Jumatatu waliyoyafanya
Simba kwenye Viwanja vya
Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam (UDSM), Kiiza
alifanya mazoezi lakini
mara kwa mara daktari wa
timu hiyo, Yasin Gembe,
alikuwa akimwambia awe
makini ili asijitoneshe.
Kocha mkuu wa kikosi hicho,
Muingereza, Dylan Kerr,
aliliambia gazeti hili
kuwa, hawezi kumlazimisha
Kiiza kucheza mechi ya leo
kwani anajua hatari ya
kumchezesha mchezaji mwenye
majeraha.
“Kiiza bado hajawa fiti kwa
asilimia mia, hivyo siwezi
kumlazimisha kucheza dhidi
ya Coastal kwani najua
hatari ya kufanya hivyo kwa
mchezaji ambaye hajapona
vizuri, ninao wachezaji
wengi, hivyo nitawatumia
kama mbadala wake,” alisema
Kerr.

Na saleh jembe



Chapisha Maoni