Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


LIGI KUU YA VODACOM KUENDELEA LEO
Ligi Kuu ya Vodacom inatarajiwa kuendelea kesho
kwa michezo sita kuchezwa katika viwanja
mbalimbali, ikiwa inaingia katika raundi ya tisa
huku kila timu ikisaka ushindi wa pointi tatu
muhimu.
Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam, Simba SC
watawakaribisha Coastal Union kutoka jijini
Tanga, mchezo utakaonza majira ya saa 10:30
jioni, huku Ndanda FC wakiwa wenyeji wa Stand
United uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini
Mtwara.
Wachimba Almasi wa Mwadui FC
watawakaribisha Yanga SC katika uwanja wa
Kambarage mjini Shinyanga, Toto African
watakua wenyeji wa maafande wa Mgambo
Shooting katika uwanja wa CCM Kirumba jijini
Mwanza.
Wakata miwa wa Turiani, Mtibwa Sugar watakua
wenyeji wa Kagera Sugar katika uwanja wa
Manungu Complex mkoani Morogoro, huku
watoza ushuru wa jiji la Mbeya katika uwanja wa
Sokoine Mbeya City watakua wenyeji wa Majimaji
kutoka mkoani Ruvuma.
Ligi hiyo itaendelea siku ya Alhamis kwa michezo
miwili kuchezwa, Tanzania Prisons watakua
wenyeji wa African Sports katika uwanja wa
Sokoine jijini Mbeya, JKT Ruvu watakua wenyeji
wa Azam FC katika uwanja wa Karume jijini Dar
es salaam.
Baraka Kizuguto
MEDIA & COMMUNICATION OFFICER
TFF



Chapisha Maoni