Ads (728x90)

Inaendeshwa na Blogger.


Shirikisho la Soka Tanzania
(TFF) limetangaza viingilio
vya mchezo wa Jumatano kati
ya Tanzania (Taifa Stars)
dhidi ya Malawi (The
Flames) kuwa ni shilingi
elfu kumi tu (10,000)
katika mchezo huo wa
kuwania kufuzu kwa fainali
za kombe la Dunia mwaka
2018 nchini Urusi.
Viingilio vilivyotangazwa
leo ni kiingilio cha juu
kabisa kwa mchezo huo
shilingi elfu kumi (10,000)
kwa viti vya VIP B & C,
huku viti vya rangi ya
chungwa, bluu na kijani
ikiwa ni shilingi elfu tano
(5,000).
Stars inayonolewa na kocha
mzawa Charles Boniface
Mkwasa imeendelea kujifua
katika viwanja vya Gymkhana
na uwanja Taifa jioni
kujiandaa mchezo huo wa
Jumatano dhidi ya Malawi,
huku wachezaji wakiwa wenye
ari na morali ya hali ya
juu kuelekea kwenye mechi
hiyo.
Wachezaji 22 wapo kambini
akiwemo mshambuliaji Mrisho
Ngasa anayecheza soka la
kulipwa nchini Afrika
Kusini aliyeripoti jana
mchana kambini, huku
wachezaji wawili Mbwana
Samata na Thomas Ulimwengu
wakitarajiwa kujiunga na
wenzao leo wakitokea
Lubumbashi – Congo DR.
Wakati huo huo timu ya
Taifa ya Malawi (The
Flames) imewasili nchini
jana saa 4 asubuhi na
kufikia katika hoteli ya De
Mag iliyopo Mwanayamala,
ambapo kikosi hicho leo
kimefanya mazoezi asubuhi
katika uwanja wa Boko
Veterani.
Waamuzi wa mchezo huo
kutoka nchini Somalia,
kamisaa na mtathimin
waamuzi wa wanatarajiwa
kuwasili leo nchini na
kufikia katika hoteli ya
Protea iliyopo Oysterbay.
Mwamuzi wa kati ni Hagi
Yabarow Wiish (Somalia),
akisaidiwa na Hamza Hagi
Abdi (Somalia), Salah Omar
Abubakar (Somalia), mwamuzi
wa akiba Bashir Olad Arab
(Somalia), mtathimini wa
waamuzi Sam Essam Islam
(Misri) na kamisaa wa
mchezo ni Muzambi Gladmore
(Zimbabwe).



Chapisha Maoni